Wale tuliopanga malengo Januari na hatujatimiza tukutane hapa, mwaka unaisha huu

Wale tuliopanga malengo Januari na hatujatimiza tukutane hapa, mwaka unaisha huu

Walau nimefanikiwa kwa 80% naamin siku zilizobak walau nitafikia 90%/Namshukuru Mungu .
 
Tuendelee kumshukuru Muumbaji kwa yote
2018 inakuja

Ushauri
Malengo yapangwe kulingana na kipato na yawe yenye uhalisia

Unaweza kuyanga ktk maeneo matano
1. Elimu ....kuongeza elimu

2. Kazi ...kupanda cheo au kufungua au kuboresha biashara

3. Family ...kuwa na familia au kupata mtoto

4. Akiba ya fedha mwisho wa mwaka

5. Nyumba au kiwanja
Mkuu mbona hujaweka gari
 
Alhamdulillah...nami sipo nyuma katika uzi huu..hakika Allah katenda ya kheri kwangu kwa huu mwaka...miongoni mwa malengo yangu ya msingi yametimia kwa mwaka huu...
1) Kupata Ajira ya uhakika
2) Kununua usafiri (pikipiki aina ya passola) wangu binafsi wa kurahisisha route za hapa na pale mjini

Panapo uhai na uzima kwa mwaka 2018 inshaallah n biidhnillah haya ndo ningependa niyafanikishe japo kwa 85%

1)Kununua Kiwanja cha Nyumba
2)Kuoa,nitaanza na kupanga kwanza
3)Kuchukua Mkopo Bank, kiasi fulani kitaingia kwenye ujenzi wa Nyumba,kiasi kumuongezea mtaji wa biashara bimkubwa na kiasi kufungua kabiashara binafsi ambapo wife ndo atakuwa anasimamia show
4)Kwenda nje ya nchi japo kwa wiki 2 kung'arisha macho kidogo japo hapo kwa Madiba (S.A) panatosha.

Oh, Allah may you easen my ways and make my dreams n plans successful in 2018...amin!
 
January moja 2017 ilinikuta na shilingi 200,000 tu. Nikiwa nyumba ya kupanga ya shilingi 70,000/= chumba na secure. Nikajiapiza December lazima nihamie kwangu. Ila mpaka apa. Nimeishia kununua Suzuki Keri na kuishi nyumba ya kupanga ya 300,000/= na balance ya cash money milioni 4. Miaka yangu ni 40 sasa.
 
Umetisha sana
 
Back
Top Bottom