Wale tulioshindwa kutimiza malengo kwa mwaka huu

Wale tulioshindwa kutimiza malengo kwa mwaka huu

Stayfar

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2016
Posts
1,088
Reaction score
2,287
Niliuanza mwaka kwa malengo ya kuacha pombe. Haukuisha mwezi nikaendelea. Nikijiwekea lengo kujenga vyumba kupangisha, ikaja mipango mingine mingi, nikaachana na ujenzi. Nikapanga kuongeza ng'ombe wa maziwa shambani kutoka 11 hadi 20, ndio kwanza wamebaki 3. Sijui nimekwamaje. Hebu na nyie wenzangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Teh teh ndivyo ilivyo mkuu. Mimi nilipanga kukamilisha nyumba na kuamia kipindi hiki cha xmass lakini nimeangukia pua kwa kushindwa kukamilisha mfumo wa maji taka wa nnje tu na kila nikiweka mipango wa kupata fedha inaota mbawa.
 
Back
Top Bottom