Wale tuliosoma Makongo Secondary School tukutane hapa

Wale tuliosoma Makongo Secondary School tukutane hapa

Kila nikisikia jina la Makongo sekondari namkumbuka mzee Tilia!, gwiji wa kemia. Tunammisi sana sasa kwenye semina za waalimu za kila mwaka!
 
Second Master Major Yeyeye! Alikuwa bandidu na Jeep yake.
 
Kwahiyo lebo ni kijani tu ?
Enzi zangu kulikuwa na Form 1 A hadi G halafu shift mbili

Form 3 na 4 kulikuwa na darasa linaitwa H kama nimekosea walisoma vichwa tu yaani waliokuwa wanaongoza Form 1 hadi 2 kisha waliingia hapo
Hilo darasa ilikuwa ukipata wastani wa 65 unajikuta hata # 20 haupo wakati darasa lingine
 
Huyu jamaa ndio mkono wake wa kulia kama umepinda flani hivi right...?

Dah, jamaa anachapa kama ndio huyo aisee. Halaf alikuwa sio mtu wa kuongea ila ukiingia kwenye 18 zake ni shida aisee.
Ushawahi kupata mkasa wa huyo Meja Kisarika?

Huyo alikuwa ni kikosi cha wanaanga yeye na akina Meja Mstaafu Alex Ndeki aliyekuwa Mkuu wa Airwing pamoja Captain Ulomi. Awali kabla mkasa huo walikuwa ni Makanali.

Walikumbwa na mkasa wa kuiba ndege ya kikosi, waliposhtukiwa ikala kwao wakashushwa vyeo meja wote. Mengine siwezi weka hapa jukwaani

Naishia hapa
 
Aiseee inatia faraja sana kusikia hizi stories.. Mm nimekaa miaka minne hapo.. Nimetoka 2009.
Tumekaa na Afande miraji Mpka mauti ilipomkuta na wananchi walilia vile vile walivyokua wanatoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lake.
Babu chacha mpenda mizigo.
Bila kumsahaua Afande sele sijui yule mwenye kitambi mpenda kula.
Namkumbuka major tarimo katupigisha sana pindi la computer kwenye zile lab mbili.
Master mayebe ambae walikua wanasema yuko kwenye intelligence ya jeshi.
Kanali kipingu alipokua akija assembly na sare Zake katui inspire sana.
Major mwaseba.
Kombaha alikua ana mikwara kisa alikua ananimilik kombi ya KLF.
Na wengine wengi..

Bila kusahau ukienda toilet Unakuta chata kubwa la POP2.
tuache utani nyambizi wakati wa Pepa kunaboa...

Makongo imetufundisha sana ujanja na kuchakata akili kuto ku give up maana stiki zilikua zinaanzia getini. Wanawake shika mguu mmoja Wanaume kunja ngumi.

Kuna MP Mmoja nilikua simpend juzi nikamuona kwa aziz ally kashastaafu Nusura nimpige Jiwe.

Kisonga ni Habari nyingine.. Wengine wanasema alikua mjeshi asiyevaa sare wengine wanasema raia tu.. Japo alikua anatafuna sana Dada zetu wa form 5 na 6...hasa wakiwa na. Maumbo nadhifu kwenye zile sketi zenye V
Kisonga ni ofisa nilimuacha ni Luteni
 
Ushawahi kupata mkasa wa huyo Meja Kisarika?

Huyo alikuwa ni kikosi cha wanaanga yeye na akina Meja Mstaafu Alex Ndeki aliyekuwa Mkuu wa Airwing pamoja Captain Ulomi. Awali kabla mkasa huo walikuwa ni Makanali.

Walikumbwa na mkasa wa kuiba ndege ya kikosi, waliposhtukiwa ikala kwao wakashushwa vyeo meja wote. Mengine siwezi weka hapa jukwaani

Naishia hapa
Kisalika alikuwa haongei sana lakini mtata balaaa....
 
Back
Top Bottom