Wale tuliotoka familia masikini na tukatusua kimaisha tukutane hapa

[emoji16][emoji16] Daah mnamsagia kunguni jamaa
 
[emoji3]
 
Haya maisha muacheni mungu aitwe mungu.

Miaka 3 tu ilibadilisha kabisa upepo wa maisha, nilitengeneza zaidi ya 600m.

Katika utafutaji naamini kabisa na bahati inachangia, sikutumia nguvu kubwa sana katika utafutaji wangu na wala simjui mganga.

watu mpaka leo hawaamini mimi kuishi kwenye nyumba ya zaidi ya 200m.
 

Mafanikio ya mtoto wa masikini yana thamani na uzito mara mia ukilinganisha na mafanikio ya mtoto wa kishua.

Yaani mpaka mtu unamaliza chuo tayari una elimu zaidi ya mtoto wa tajiri aliyehitimu na wewe.

Watoto wa matajiri maranyingi wanabebwa na majina ya wazazi wao, hata akienda kukopa benki akitaja ubini wake tu, anasomeka na kuaminiwa. Sisi kajamba nani misukosuko zaidi ya mia.

Mimi hata kumaliza sekondari ilibidi nijilipie ada. Chuo ilibidi niingie mtaani nizichange kwanza ndo nikajisomesha baada ya miaka mingi toka nimalize sekondari.

Umasikini siyo sifa ila nguvu, maarifa, kujitoa na ujasiri tunaowekeza katika kujikwamua ukilinganisha na tulipotoka, hakika unashangaa wakati mwingine mtu umetoboaje. Na wanaokujua yamkini wengine walikudharau wanashindwa kuamini kama kweli ni wewe.

Changamoto sasa inatokana na hayo mafanikio, utayapokeaje binafsi, wengine wanaitumia kama fursa ya kuonyesha umwamba mitaani kwa kuwekeza kwenye vitu visivyo na tija kama magari ya kifahari au vitu vya thamani badala ya kuwekeza kunakomhakikishia kesho yake. Hapa ndo unakuta baada ya muda mfupi wengi tunarudi kwenye umasikini japo siyo kwa kiwango kile cha awali.

Ni vema mtu ukitusua ukakumbuka jana yako na kujiwekea mikakati ya kulinda kesho kwa njia zote. Hii ni kutokana na kwamba leo tunazipata lakini inawezekana kesho tukakuta ile mirija imefungwa au chochote kinaweza tokea ukashuka.

Tujipange na tulinde kesho yetu.
 
Usije ukajisahau watoto wakawa Type B kama ilivyokuwa kwa wazazi wako!
 
Ahhahahahahahhaha! Mkuu utakuwa ulibet zile "beti kichaa"! Sheriff kumfunga Real Madrid away na over ya 2.5! Ahahahahahahahah!!
 
Ahsante sana, upo huru kuwaza chochote.
Hujamaliza hata nusu mwaka tangu ujiunge JF lakini unataka kuanza uongo na utapeli. Hii thread yako unataka watu wakuombe connection maana unasema wewe ni meneja at the same time ni Mkurugenzi tena wa bodi.

Acha ushamba dogo, jiandae na September Conference. Ulidhani huku ni facebook?
 
Huyu dogo ni tapeli kama hamjashtuka. Na juzi tu alivutwa mapumbu na mke wake kwaajili ya huu ujinga wake.
 
Kwanini mkifanikiwa mnakua na roho mbaya sana
 
Tupe mbinu mkuu, ulifanyaje au mishe gani hizo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…