Nakumbuka nilikua likizo fupi wakati nasoma Mazengo Dodoma nilikuja Dar. Ni kipindi kile cha ulanguzi wa sigara na vitu kama hivyo. Basi mimi nilishukia kwa dadangu Kinondoni na kwa vile nilikua na ule mchemko wa ujana na kutaka kuonyesha kwamba hata mimi nipo, niliamua kuwafuata wanandugu Magomeni Kagera.
Pale palikuwa na mtoto wa kakaangu akanitaka tuingie kijueni kupata hili na lile. Nilimkubalia na wakati tunakunywa ghahawe kijiweni pale Magomeni Kagera njia panda Mburahati, nakumbuka ilikua kama saa moja na nusu hivi nilishtukia kundi la mapolisi na mikoti yao wakifoka kuwa "mko chini ya ulinzi" kisa eti ninyi ni walanguzi wa sigara.
Tulifungwa mashati vijana wote tukapelekwa mzobwe hadi polisi Magomeni. Sijui hili wala lile naona tunaingizwa kwenye ukumbi wenye mama ntilie kibao, mie nikajua labda jamaa kwa huruma yao wameamua kutupiga chipsi. Mara ghafla nasikia haya chuchumaa chini wote. Anza kuruka kichura, walahihi tulihenyeshwa hadi saa nane usiku ndio wanaanza kutuandikisha maelezo.
Nilitoa kitambulisho cha shule na kuwaeleza mie pale nilienda kunywa gahawa tu, ni mara yangu ya kwanza kuja Dar. Polisi waliniambia sina jinsi ila kulala sero hadi asubuhi ndo nichape zangu lapa.
Siku ile nakumbuka yaani toka tukamatwe hadi asubuhi niliona kaa siku saba. Miongoni mwa tuliokua nao waliwalipia polisi chakula pale kwa mama ntilie na waliachiwa waende zao. Masikini mie nilikua walau hata kile polisi walicholipiwa na mie niunganishwe maana ubao niliokua nao sii haba.
Polisi kwa huu ubaguzi wa aliye nacho na asiye nacho Mungu anawaona mjue...
Sent using
Jamii Forums mobile app