Wale tuliowahi kukutana na mikasa ya polisi, andika chochote kujikumbusha maumivu

Wale tuliowahi kukutana na mikasa ya polisi, andika chochote kujikumbusha maumivu

Wakuda hawa walinikamata siku moja tabata wakanileta hadi dodoma centra y'a Dom chafu kishenzi alafu maafande wakatili kinyama siwapendi police

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sita sahau ilikuwa 2006 nikiwa o level niliaga hom naenda camp kupiga msuli kumbe nina promise na mtoto mzuri wa mtaa wa pili ilenavuka tu barabara uso kwa uso na defender kumbe jamaa walikuwa kwenye patrol mala sauti simama hapohapo!! maafande wakashuka ikabidi niwe mpole nikawambia minimwanafunzu washkaji hawakuelewa kilichonisaidia nilikuwa na kadi ya chama pendwa.Baada ya kusalimika popote napokuwa lazima niwe na kadi pendwa maana imekuwa mwokozi wangu
Ningeenda selo hivihivi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilisha wahi kusimamishwa na askari akanihoji kuhusu maswala ya barabarani akakagua gari hakukuta tatizo ila mwishowe aliniambia KWAKUA AMENISIMAMISHA NA HATA KAMA SINA TATIZO HAINA MAANA ATANIACHIA HIVIHIVI HIVYO NIJONGEZE nikampa elfu 5 AKAGOMA ANATAKA 10 baada ya dk kama 40 nikaona ntachelewa ikabd nimpe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilikamatwa Na Bange border nikawekwa lockup. Na ilikuwa a week to my wedding.

Humo lockup asikuambie mtu. Harufuuuu mbaya ya mikojo, cold floors. Lol.
Jaman, kumbe bulaya hakuigiza bure
Nilikamatwa Na Bange border nikawekwa lockup. Na ilikuwa a week to my wedding.

Humo lockup asikuambie mtu. Harufuuuu mbaya ya mikojo, cold floors. Lol.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka nilikua likizo fupi wakati nasoma Mazengo Dodoma nilikuja Dar. Ni kipindi kile cha ulanguzi wa sigara na vitu kama hivyo. Basi mimi nilishukia kwa dadangu Kinondoni na kwa vile nilikua na ule mchemko wa ujana na kutaka kuonyesha kwamba hata mimi nipo, niliamua kuwafuata wanandugu Magomeni Kagera.

Pale palikuwa na mtoto wa kakaangu akanitaka tuingie kijueni kupata hili na lile. Nilimkubalia na wakati tunakunywa ghahawe kijiweni pale Magomeni Kagera njia panda Mburahati, nakumbuka ilikua kama saa moja na nusu hivi nilishtukia kundi la mapolisi na mikoti yao wakifoka kuwa "mko chini ya ulinzi" kisa eti ninyi ni walanguzi wa sigara.

Tulifungwa mashati vijana wote tukapelekwa mzobwe hadi polisi Magomeni. Sijui hili wala lile naona tunaingizwa kwenye ukumbi wenye mama ntilie kibao, mie nikajua labda jamaa kwa huruma yao wameamua kutupiga chipsi. Mara ghafla nasikia haya chuchumaa chini wote. Anza kuruka kichura, walahihi tulihenyeshwa hadi saa nane usiku ndio wanaanza kutuandikisha maelezo.

Nilitoa kitambulisho cha shule na kuwaeleza mie pale nilienda kunywa gahawa tu, ni mara yangu ya kwanza kuja Dar. Polisi waliniambia sina jinsi ila kulala sero hadi asubuhi ndo nichape zangu lapa.

Siku ile nakumbuka yaani toka tukamatwe hadi asubuhi niliona kaa siku saba. Miongoni mwa tuliokua nao waliwalipia polisi chakula pale kwa mama ntilie na waliachiwa waende zao. Masikini mie nilikua walau hata kile polisi walicholipiwa na mie niunganishwe maana ubao niliokua nao sii haba.

Polisi kwa huu ubaguzi wa aliye nacho na asiye nacho Mungu anawaona mjue...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Walinidabua na picha za gomba kwenye simu, muhuni nikiwa nachanja na wanangu mageto...wakataka wanitie ndichi na niwapeleke wakawachukue wana. Nikaona sio kweli siwezi kuwachoma wahuni nikawahonga laki mapoti wakanitema. Ila nilizunguka kwenye PT toka saa4 mpk saa 10 full stress.
 
Kubebwa kama gunia na virungu vya kutosha kuingia mahabusu yenyewe ilikuwa ni mikikimikiki mara nimeshika kiti mara mlango!
hahahaah hadi nimecheka sana hapa pole san mkuu
 
Bro Wangu alikua amelewa akaanza kusumbua home nikampa kichapo laana nakumbuka jion yake nimechill geto sister alikuja na mapai wakanipiga pingu kwenye tax hadi kituo cha ungalimited nilichezea kichapo laana
Kule sero nlikutana na Chalii mmoja tukaanza kuzipiga ilikua ni shida full baridi,mbu just like hell
Kesho asubuh tulipigishwa usafi apo kituoni
Kabla maza hajaja kunitoa
Paka Leo namsalimiaga sister basi tu
Ni muuaji
 
Back
Top Bottom