Wale tunaopenda vacation, sehemu gani ya utalii Tanzania uliyofika au unatamani kufika?


Au Airbnb badala ya hoteli
 
Kuna kahotel kamoja kako Bagamoyo kanaitwa Firefly niliendaga na famikia Christmas [emoji319] moja. Tulienjoy sana

Ukitaka kuiona tazama wimbo wa Marioo - Ifunanya wameshuti pale.
Gharama zao.....?
 
Mkoa wa Mbeya mtu atembelee wapi na wapi
Kuna maeneo kadhaa mazuri ya kutembelea mkoani Mbeya, jumlisha na mkoa wa Songwe
  1. Kawetire view point - Njia ya kwenda Chunya. Pale utaona bonde la ufa kwa ukubwa wake, yaani ile trough (beseni) la bonde la ufa, ni sehemu nzuri sana. Iko njia kuu ya kwenda Singida na Tabora eneo la Kawetire
  2. Daraja la Mungu, likpo Rungwe Mbeya. Ni mwamba mgumu (jiwe) ambao umevuka mto na pana mandhari nzuri sana ya kuvutia. Jirani na hapo pana kijungu (maji ya mto yanapotelea ardhini)
  3. Tembelea Matema, fukwe za ziwa Nyasa. Kuna fukwe nzuri sana na utapata nafasi ya kuogelea ziwani, maji baridi burudani kabisa na utapata nafasi ya kula samaki wa ziwa Nyasa
  4. Eneo la Songwe (Majimoto) kuna majimoto (geysers) yanayotoka ardhini. Maji ni ya moto kiasi unaweka yai linaiva na unakula. Kijiji kipo kilometa 8 kutoka uwanja wa Ndege wa Songwe, kama unaelekea Tunduma
  5. Ukipata nafasi temebelea kimondo cha Mbozi, eneo la Ndolezi, nao ni utalii tosha.
  6. Mwisho, tembele mbuga ya maua ya Kitulo, ni mwendo wa saa 2 kutoka Mbeya mjini, uelekeo wa Makete Njombe kupitia Igoma.
 
Natamani kuona Wildebeest Migration....
Masai Mara au Serengeti....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…