Wale tunaovaa Barakoa tupeane experience jinsi ya Kuvaa, mwenzenu inaniletea matatizo

Wale tunaovaa Barakoa tupeane experience jinsi ya Kuvaa, mwenzenu inaniletea matatizo

Ndugu zangu watanzania tupo ktk janga la Corona na Wizara ya Afya imetoa njia za kujikinga na janga hili ikiwa ni pamoja na uvaaji wa barakoa ktk sehemu za mikusanyiko.

Lakini jambo la kushangaza baadhi yetu wanavaa barakoa lkn unakuta barakoa ipo chini ya kidevu au barakoa imejaa mdomoni, tena unakuta mtu mzima anavaa barakoa kisanii

Tuache masihara tutapuputika kama tunapuuza.

tuchukue tahadhari korona inaua.
 
Barakoa za ndani za vitambaa inafuliwa toka October 2019 ilianza corona bado mhusika anaitumia.
 
Ingetolewa elimu ya uvaaji wa barakoa,usafi wa mikono,inapaswa kubadilishwa mara ngapi,kama ya kitambaa inasafishwa vipi n.k
 
Sio kuwa hawajui matumizi ya barakoa ila wanavaa kama fashion mkuu.

Hii ni kwa sababu ugojwa wa Corona umekuwa kama popo bawa. Utasikia tu alipita hapa, jana alikuwa kule. Ukienda kuwauliza wahusika wa eneo lile nao hawajui wanasikia alikuwa ulipotokea wewe.

Corona imekuwa kama changa la macho. Mtaani kwako huoni wanaochukua tahadhali na misiba huoni. Ugonjwa umebakia vinywani mwa wanasiasa.
 
Juzi Mo Dewji anaulizia namna ya 'kumetchisha' barakoa na nguo ili tu apendeze…. tajiri jinga kabisa.
Kuna mwanangu alikua anakubali sana mo na alikua role model wake, na jamaa alikua hamkubali mondi balaa. Sasa ile mo kaenda studio za wasafi na kuanza kucheza singeli jamaa alimshusha vyeo vyote😁😁.

Hawa watu mashuhuri kuna namna inabidi wabehave wanaangaliwa na wengi sana.
 
Salaam wakuu,

Huu Ugonjwa wa Corona umekuja na mengi ikiwemo kuvaa Barakoa kuziba mdomo na Pua ili ili majimaji ya Korona yasikupate au hata kama na wewe una Corona usiweke kuambukiza wengine pale unapo piga chafya.

Ila mimi nikiivaa naona ni Mateso makubwa. Wenzangu mnawezaje kuvaa Barakoa asubuhi hadi jioni?

Mimi nikivaa Barakoa muda mrefu, kichwa kinaniuma, nasikia kizunguzungu, macho yanakua hayaoni vizuri, na saa nyingine najisikia homa pae nivaapo Barakoa kuliko siku ambazo Sivai.

Imefika kipindi hata kuvaa najishauri naiweka mfukoni tu. Tena bora ya Kitambaa hizi za kushona, lakini nikivaa vile Special ndo najisikia kufa kabisa.

Nimekuja hapa kuuliza kama ni mimi tu au kila mtu anajisikia kama mimi? Kama vipi tushinikize Shirika la Viwango Tanzania Bureau of Standards (TBS) lifanyie uchunguzi hizi barakoa Zilizoingia Nchini. Naamini hazina viwango. Sababu ukiwa umeivaa ukipumua hewa haitoki nje, ukivuta unavuta hiyo hiyo. Nahofia Barakoa zinaweza niletea maradhi hivyo nina panga kufanya kinyume labda nishauriwe namna nzuri ya kuvaa.

Tangu nianze kuvaa Barakoa Macho yangu yamekua mekundu kama navuta Kaya. Ni mateso kwa kweli, Mungu tuokoe.

Nakosa uhuru wa kuvuta hewa safi. Pumzi ninayo ivuta hainitoshi. Kama nilikua navuta pumzi ya kujaza lita moja, sasa navuta kikombe kimoja tu nikiwa nimevaa Barakoa aka Mask

Leo nmeona idadi ndogo ya watu walovaa Barakoa, nahisi wamekiona cha moto.

Waziri wa Afya alikataza tusivae Barakoa namba N95 sababu ni chache na tuwaachie wahudumu wa afya. Kwakuwa hili swala linahusu uhai, imebidi nitafute hizi kwani nahisi zitakuwa na ubora zaidi.

View attachment 1431952
Mdomoni barakoa chini condom
 
kama una changamoto za kupumua ndio unapaswa ung'ang'ania kuvaa barakoa haswa, maaana ukijifanya unashusha barakoa chini ya kidevu kutoa pua lako nje uvute hewa hapo ndipo unavuta kirusi cha korona awamu ya 3.
lkn kuna wengine wanauza sura![emoji1787]
hivi inawezekanaje unauza nyago mbele ya kifo? hivi unawezaje kuhatarisha uhai wako kwa kisingizio cha kukosa hewa?
hivi kweli ndugu zangu watanzania hayo ni maarifa au?!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom