Wale wa home made products, njooni hapa

Wale wa home made products, njooni hapa

Kwa namna maarifa yanavyozidi kuongezeka kuna bidhaa nyingi zinaweza tengenezwa ukiwa nyumbani tu kikubwa ujikusanyie malighafi Kwanza. Mimi binafsi nmejifunza vitu vingi na nisingependa kuwa mbinafsi, naweza kushare baadhi ya maarifa niliyonayo hapa, najua wengi wanajua pia, ukiona yafaa waweza weka maarifa yako hapa from scratch au hata video ikiwezekana.

Mfano wa maarifa hayo ni pamoja na utengenezaji wa:- sabuni zote kwa formula zote, shampoo, mishumaa, tomato soes, maji ya betri, mchanganyo wa dawa za kuprintia t-shirts, dawa za viatu, dawa za meno, mafuta ya kujipaka, lotion, spray, dawa za kusafisha malumalu, cake, pombe, wine, spirits, soda n.k, najua wengi wana wengi

Karibuni wana jukwaa


NITAANZA NA SABUNI YA MAJI

Ni sabuni nzuri kwa ajili ya matumizi ya kufulia, kudekia na kufukuzia wadudu.

Mahitaji yote yanapatikana kwenye maduka ya vjfaa vya wajasiliamali au waweza tafuta ofisi za Allied Chemicals au SIDO na kwa wale wa Mwanza tuwasiliane ili nikuelekeze..

MAHITAJI
kwa sabuni lita 25

✓chumvi yeyote kilo 1
✓ sulphonic acid ½ lita
✓Siles kilo 1
✓Rangi (uipendayo) vijiko viwili vya chakula
✓perfume (uipendayo) Mili-lita
50
✓maji lita 25
✓diaba la plastic (sio chuma)
✓mti mkavu wa kukorogea

HATUA ZA UTENGENEZAJI
Tanabahi: hii ni formula mpya, kama ipo nyingine nzuri zaidi na rahisi utaweka.

¶ baada ya kuweka maji kwenye diaba hizo lita 25 weka chumvi yote (kilo 1) kisha koroga dkk 5 na uhakikishe imeyeyuka yote

¶ Kisha tia sulphonic Acid {hakikisha umevaa gloves au kilinda mikono chochote ili tu sulphonic isikumwagikie (ni hatar ikikumwagikia)} kisha koroga kwa nusu saa nzima mpaka uone povu jeupe limeshamiri kwenye maji

¶ kisha weka Siles na koroga vizuri kwa nusu saa nyingine mpaka sabuni iwe nzito kabisa na baada ya hapo funika diaba lako na liache kwa masaa kumi na mbili kuruhusu mchanganyo ukae sawa

¶ Baada ya hapo waweza funua na kutia perfume kisha koroga dkk 5 na kisha weka rangi then koroga tena dkk 5, na sabuni itakuwa tayr kwa matumizi

tanabahi: usiache wazi muda mrefu ili kutunza perfume yako na usiiache juani, karibuni kwa maswali.
Hii shule tunaipata JF tu, hongera kwa ubunifu na kushirikisha hapa
 
NAMNA YA KUTENGEZA DAWA YA KUNG'ARISHA VIATU UKIWA NYUMBANI

kuna njia lukuki za kutengeneza mng'arisho wa viatu, ninapendekeza njia tatu (3) hizi kwa ajili ya matumizi ya nyumbani tu sio biashara, mfunze mwanao njia mbadala ya kuyakabili maisha

NJIA YA KWANZA- Ganda la ndizi

Tanabahi:-Nitakuwa straight kidogo kufanya mambo kuwa rahisi, kama una swali utauliza

Ukimenya ndizi mbivu kwa ajili ya kula, lile ganda lile ni polisher nzuri sana, sasa ile sehemu nyeupe ya ndani itumie kufutia kiatu chako (viatu vya leather inafaa zaidi) viache kwa dkk 10 kisha tafuta kitambaa kikavu cha cotton nyepesi kisha futa kiatu chako na kitakua na mng'ao murua kabisa


NJIA YA PILI-mafuta ya zeituni na juice ya limao

Kwa vifaa tajwa hapo juu, hakikisha mafuta ya zeituni ni yale ya dukani na juice ya limao iwe ile ya dukani isiwe ile ya kukamua mwenyewe (sio lemonade)

Uwiano uwe 2:1 yaani ukichukua vijiko vinne vya zeituni weka vijiko viwili vya limao

Baada ya kuchanganya acha mchanganyiko utulie kisha unafaa kwa ajili ya kung'arisha kiatu, sasa chukua kitambaa safisha kiatu chako kitoke vumbi lote kisha chukua mchanganyo wako sasa chovyea kwa kitambaa (chovya kidogo tu) Kisha anza kufuta kiatu chako na baada ya hapo tumia sponji au kitambaa laini cha pamba kufuta (kutengeneza mng'ao) then enjoy your shoes[emoji108]


NJIA YA TATU NDIO KIWI YENYEWE nitaiweka sio muda mrefu Sana..enjoy your home made products
View attachment 1707814View attachment 1707816
 
JINSI YA KUTENGENEZA LOTION ASILIA KWA NGOZI NYORORO YENYE MNG'AO (NATURAL)*

Chagua moja kati ya lotion zifuatazo

Mahitaji

✓Vitamin c powder (kijiko 1 cha chakula)

✓Vitamin e Capsule (kidonge 1)

✓Rose water (kijiko 1 cha chakula)

✓Glycerin (kijiko 1 cha chakula)

✓Shea butter au Vaseline lotion/Lotion yoyote uipendayo 100ml

HATUA ZA KUFUATWA

Tia rose water kwenye bakuli safi kisha tia kijiko kimoja cha unga wa vitamin C

Changanya vizuri na ukoroge kwa muda wa dakika 5 mpk vitamin c iyeyuke kabisa kisha ongezea glycerin na vitamin e na uchanganye vizuri

Tia lotion yako ya vaseline ujazo wa ml 100 ama shea butter ama cream yoyote uipendayo mwenyewe kisha changanya vizuri hadi ichanganyike

Weka kwenye chupa safi tayari kwa matumizi

Hii itafanya ngozi yako kua laini na kuondoa ukavu wa ngozi pamoja na kuiacha ikipendeza zaidi na zaidi

Unaweza kupaka kwenye mwili hata usoni na ni salama kabisa haina sumu

Note: hapa huanzi from scratch kutengeneza lotion lakini unapata uhakika wa kung'arisha ngozi yako within a week, kwa viambata tajwa hapo ukichanganya na lotion yoyote, preferably Vaseline
Vitamin C inapatikana wapi
 
Santee sana mkuu, hizi ni products ambazo msingi wake lazima uanzie nyumbani, ziwe miongoni mwa zile shughuli muhimu za nyumbani, mwagize mwanao tu akatengeneze dawa ya viatu au ya meno au mafuta ya kujipaka n.k.
Nilichogundua hapa mkuu ni ujuzi upatikane...baada ya hapo ni kutafuta vitendea kazi na kuzalisha kibiashara
 
Na kama unafahamu kutengeneza na sabuni za Mchele naomba formula.
 
Asante, na ile kojic powder unaifahamu pia .
Yeaah, ni unga special hutumika kwa ajili ya kung'arisha ngozi, kuondoa mabaka na chunusi pia, kama unahitaji basi nakuunganisha na huyu, anao mwingi tu, yuko Mwanza ukihitaji mikoani atakutumia bila shida yeyote.

0767388666
 
Na Kama unafahamu kutengeneza na sabuni za Mchele naomba formula.
MALIGHAFI

✓Maji ya mchele
✓kaustiki soda
✓mafuta ya mise au Nazi

Hatua ya kuandaa

Andaa ndoo Lita 20 weka maji yalio oshewa mchele kwenye ndoo Lita 4

Kisha weka kaustiki soda nusu kilo kisha koroga kwa muda Wa dakika 5 kisha hifadhi sehemu salama kwa muda Wa siku 2 hadi 3

Baada ya siku 3

Anza kuchemsha mafuta ulionayo kama ya Nazi au mise au ya mawese hakiksha yanapata moto na kua na vuguvugu (yasichemke sana)

Baada ya hapo kata kidumu cha Lita 5 kwa juu kisha weka maji Yale ya mchele ulio changanya na kausti weka nusu Lita kisha weka mafuta yako Lita moja kisha koroga kwa haraka na muda mfupi utaona mchanganyiko Wako umekua mzito kama uji

Mimina na utie katika umbo na acha ikauke

Itakauka kwa muda wa masaa 6 hadi 8

Baada ya kukauka utapata sabuni ambayo inaondoa vipere usoni na kuacha uwe nyororo kabisa
 
Yeaah, ni unga special hutumika kwa ajili ya kung'arisha ngozi, kuondoa mabaka na chunusi pia, kama unahitaji basi nakuunganisha na huyu, anao mwingi tu, yuko mwanza ukihitaji mikoani atakutumia bila shida yeyote.

0767388666
Asante nitamtafuta.
 
Hapo kwenye ndoo sijaelewa
Kuna dhana tatu hapo 1.ndoo ya plastic 2.maji ya mchele lita 2 3.koustic soda.

Maelezo.

Ni marufuku, kutumia chombo chenye asili ya chuma kuyeyusha koustic kwa sababu kitayeyuka chenyewe, tumia ndoo au chombo cha aluminium au plastic hasa plastic.

Kuyeyusha koustic nusu kilo unahitaji maji lita nne, hivyo baada ya kupata mchanganyo kwa hizo siku 2 au 3 na kutoa kiasi unachohitaji utatunza inayobaki kwa ajili ya matumizi ya wakati mwingine au la utaimwaga tu.
 
Back
Top Bottom