Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Check pharmacy kubwa au cosmetics shop utapata ukikosa nambie nitakutumiaAsante mkuu, nimekubali uzalendo wako...barikiwa sana.
Unga wa vitamin C unapatikana wapi?
Hii shule tunaipata JF tu, hongera kwa ubunifu na kushirikisha hapaKwa namna maarifa yanavyozidi kuongezeka kuna bidhaa nyingi zinaweza tengenezwa ukiwa nyumbani tu kikubwa ujikusanyie malighafi Kwanza. Mimi binafsi nmejifunza vitu vingi na nisingependa kuwa mbinafsi, naweza kushare baadhi ya maarifa niliyonayo hapa, najua wengi wanajua pia, ukiona yafaa waweza weka maarifa yako hapa from scratch au hata video ikiwezekana.
Mfano wa maarifa hayo ni pamoja na utengenezaji wa:- sabuni zote kwa formula zote, shampoo, mishumaa, tomato soes, maji ya betri, mchanganyo wa dawa za kuprintia t-shirts, dawa za viatu, dawa za meno, mafuta ya kujipaka, lotion, spray, dawa za kusafisha malumalu, cake, pombe, wine, spirits, soda n.k, najua wengi wana wengi
Karibuni wana jukwaa
NITAANZA NA SABUNI YA MAJI
Ni sabuni nzuri kwa ajili ya matumizi ya kufulia, kudekia na kufukuzia wadudu.
Mahitaji yote yanapatikana kwenye maduka ya vjfaa vya wajasiliamali au waweza tafuta ofisi za Allied Chemicals au SIDO na kwa wale wa Mwanza tuwasiliane ili nikuelekeze..
MAHITAJI
kwa sabuni lita 25
✓chumvi yeyote kilo 1
✓ sulphonic acid ½ lita
✓Siles kilo 1
✓Rangi (uipendayo) vijiko viwili vya chakula
✓perfume (uipendayo) Mili-lita
50
✓maji lita 25
✓diaba la plastic (sio chuma)
✓mti mkavu wa kukorogea
HATUA ZA UTENGENEZAJI
Tanabahi: hii ni formula mpya, kama ipo nyingine nzuri zaidi na rahisi utaweka.
¶ baada ya kuweka maji kwenye diaba hizo lita 25 weka chumvi yote (kilo 1) kisha koroga dkk 5 na uhakikishe imeyeyuka yote
¶ Kisha tia sulphonic Acid {hakikisha umevaa gloves au kilinda mikono chochote ili tu sulphonic isikumwagikie (ni hatar ikikumwagikia)} kisha koroga kwa nusu saa nzima mpaka uone povu jeupe limeshamiri kwenye maji
¶ kisha weka Siles na koroga vizuri kwa nusu saa nyingine mpaka sabuni iwe nzito kabisa na baada ya hapo funika diaba lako na liache kwa masaa kumi na mbili kuruhusu mchanganyo ukae sawa
¶ Baada ya hapo waweza funua na kutia perfume kisha koroga dkk 5 na kisha weka rangi then koroga tena dkk 5, na sabuni itakuwa tayr kwa matumizi
tanabahi: usiache wazi muda mrefu ili kutunza perfume yako na usiiache juani, karibuni kwa maswali.
Vitamin C inapatikana wapiJINSI YA KUTENGENEZA LOTION ASILIA KWA NGOZI NYORORO YENYE MNG'AO (NATURAL)*
Chagua moja kati ya lotion zifuatazo
Mahitaji
✓Vitamin c powder (kijiko 1 cha chakula)
✓Vitamin e Capsule (kidonge 1)
✓Rose water (kijiko 1 cha chakula)
✓Glycerin (kijiko 1 cha chakula)
✓Shea butter au Vaseline lotion/Lotion yoyote uipendayo 100ml
HATUA ZA KUFUATWA
Tia rose water kwenye bakuli safi kisha tia kijiko kimoja cha unga wa vitamin C
Changanya vizuri na ukoroge kwa muda wa dakika 5 mpk vitamin c iyeyuke kabisa kisha ongezea glycerin na vitamin e na uchanganye vizuri
Tia lotion yako ya vaseline ujazo wa ml 100 ama shea butter ama cream yoyote uipendayo mwenyewe kisha changanya vizuri hadi ichanganyike
Weka kwenye chupa safi tayari kwa matumizi
Hii itafanya ngozi yako kua laini na kuondoa ukavu wa ngozi pamoja na kuiacha ikipendeza zaidi na zaidi
Unaweza kupaka kwenye mwili hata usoni na ni salama kabisa haina sumu
Note: hapa huanzi from scratch kutengeneza lotion lakini unapata uhakika wa kung'arisha ngozi yako within a week, kwa viambata tajwa hapo ukichanganya na lotion yoyote, preferably Vaseline
Santee sana mkuu, hizi ni products ambazo msingi wake lazima uanzie nyumbani, ziwe miongoni mwa zile shughuli muhimu za nyumbani, mwagize mwanao tu akatengeneze dawa ya viatu au ya meno au mafuta ya kujipaka n.k.Mada nzuri mkuu, kwa ujuzi ulio nao,unatakiwa uwe na kiwanda kidogo
Angalia maduka ya dawa za binadamu au cosmetics shops au ukiwa tayr kutengeneza nambie nikuagizieVitamin C inapatikana wapi
Nilichogundua hapa mkuu ni ujuzi upatikane...baada ya hapo ni kutafuta vitendea kazi na kuzalisha kibiasharaSantee sana mkuu, hizi ni products ambazo msingi wake lazima uanzie nyumbani, ziwe miongoni mwa zile shughuli muhimu za nyumbani, mwagize mwanao tu akatengeneze dawa ya viatu au ya meno au mafuta ya kujipaka n.k.
Asante, na ile kojic powder unaifahamu pia.Angalia maduka ya dawa za binadamu au cosmetics shops au ukiwa tayr kutengeneza nambie nikuagizie
Yeaah, ni unga special hutumika kwa ajili ya kung'arisha ngozi, kuondoa mabaka na chunusi pia, kama unahitaji basi nakuunganisha na huyu, anao mwingi tu, yuko Mwanza ukihitaji mikoani atakutumia bila shida yeyote.Asante, na ile kojic powder unaifahamu pia .
MALIGHAFINa Kama unafahamu kutengeneza na sabuni za Mchele naomba formula.
Asante nitamtafuta.Yeaah, ni unga special hutumika kwa ajili ya kung'arisha ngozi, kuondoa mabaka na chunusi pia, kama unahitaji basi nakuunganisha na huyu, anao mwingi tu, yuko mwanza ukihitaji mikoani atakutumia bila shida yeyote.
0767388666
MALIGHAFI
✓Maji ya mchele
✓kaustiki soda
✓mafuta ya mise au Nazi
Hatua ya kuandaa
ndoo Lita 20 weka maji yalio oshewa mchele kwenye ndoo Lita 4
Kuna dhana tatu hapo 1.ndoo ya plastic 2.maji ya mchele lita 2 3.koustic soda.Hapo kwenye ndoo sijaelewa
Karibu mkuuAsante Mno kwa uzi huu