Mkuu naomba formula ya kutengeneza shampoo ya nywele natural kama unayo.NJIA YA TATU
1. Chukua vijiko 2 vya baking powder
2.Weka vijiko 2 vya coconut oil
3.Weka matone 10 ya essential oil
kisha changanya vyote kwa pamoja mpaka mchanganyo uwe mwepesi (sio mwepesi Sana) utakuwa tayari kwa matumizi.
Kwa vipimo vipi mkuu? Hatuchemshi?Formula ya kutengeneza mayonnaise
Chukua mayai
Chukua mafuta ya kupika
Kitunguu swaumu
Chumvi
Changanya vyote kwenye blender
Kama uko dar mcheki, yuko mwananyamala kwa kopa amepakana na kituo cha mafuta cha ORYX, anaitwa Steve Setumbi na brand yake inaitwa PARK LAND CULTURAL GROVEhttps://www.google.com/url?sa=t&sou...FjADegQICBAD&usg=AOvVaw2A1XbGl7P4oiYbwJXH8_0Y
Ingia kwa hiyo blog ucheki designs zake huyu jamaa, kumpata fuatalilia hyo address aliyoandika humo, ni rahisi kumpata na ukitaka kujifunza mtaelewana mkuu...nikutakie ufuatiliaji mwema.
Kojic powder cheki insta kuna wabongo wanauzaAsante, na ile kojic powder unaifahamu pia .
Hii huchemshi mi natengenezaga hivi:Kwa vipimo vipi mkuu? Hatuchemshi?
[emoji120][emoji120], nashukuru mkuu ni kitu kipya, sikufaham kabla. Hapo kwenye kitunguu thomu sijakifaham bado naomba nieleweshe tafadhari.Hii huchemshi mi natengenezaga hivi:
Viini vya yai 4
Mafuta ya kupikia nusu kikombe hadi kikombe kimoja( ukipata olive oil ni bora zaidi
Kitunguu saum kiponde chota kidogo sana
Ndimu kipande 1/vinegar vijiko 3-5
Chumvi
Optionals:-
Flavors nyingine upendazo mfano unaweza ongeza mustard seeds kidogo kiasi robo kijiko cha chai Ila ukiamua kuweka hizi zitwange pamoja na kitunguu thomu.
Pilipili manga ya unga
Vifaa muhimu:
Bakuli
Kikombe chenye mdomo unaweza tumia cha kawaida pia
Uma wa plastic (huu Ni mzuri zaidi unapiga kwa wepesi na kuchanganya bila kelele) Ila unaweza tumia hata wa kawaida
Hatua:
Vunja yai moja moja tenganisha ute na viini
Chukua uma wako anza kupiga mayai kama kawaida, tia chumvi...piga.
yakishachanganyika vizuri chukua kikombe chenye mafuta anza kunyunyizia kidogo kidogo yatoke mfano wa uzi vile huku ukiendelea na shughuli ya upigaji mayai.
Endelea kupiga huku unanyunyizia mafuta Hadi uone mchanganyiko wako unakua na thick creamy texture, (ute mzito)
Stop kumimina mafuta ukiona umepata mchanganyiko unaopendeza,
Anza kuongeza viambata vingine huku ukiendelea kuchanganya vizuri, vinegar, ndimu, kitunguu thomu, pilipili manga.
Hifadhi kwenye chombo chenye mfuniko tayari kwa matumizi.
Maji ni Lita 4 ila utatumia ndoo ya plastic ya Lita 20 tupuMkuu mleta mada.Kama nimeelewa hivi
Katika kutengeneza sabuni ya Mchele Vifaa ni:-
1.Maji ya Mchele Lita 20
2.Caustic soda 1/2 kilo
3.Mafuta Lita 3.
Ni hivyo tuu? Je itakuwa na povu? Je hatuweki glycerine?
He haiwezekani kuifanya ngozi kubabuka na kuwa kavu?
Ahsante
Itakuwa na povu? Bila sulphonic acid Wala siles?Maji ni Lita 4 ila utatumia ndoo ya plastic ya Lita 20 tupu
hapana mkuu, kuwa na amani kuu, ukiishaiyeyusha coustic kwa huo muda usiopungua masaa 12 inafaa kabisa kwa matumizi, kwa sababu ni ya kuogea haitahitaji povu jingi so kwa matumizi ni makini kabisa, aidha kwa sabuni za miche huwa hatutumii sulphonic badala yake coustic soda ndiyo inatumika.Mkuu mleta mada.Kama nimeelewa hivi
Katika kutengeneza sabuni ya Mchele Vifaa ni:-
1.Maji ya Mchele Lita 20
2.Caustic soda 1/2 kilo
3.Mafuta Lita 3.
Ni hivyo tuu? Je itakuwa na povu? Je hatuweki glycerine?
He haiwezekani kuifanya ngozi kubabuka na kuwa kavu?
Ahsante
usiwe na wasiwasi mkuu, itatoaItakuwa na povu? Bila sulphonic acid Wala siles?
Endelea kufuatilia mkuu, nitaweka mada hii sio muda mrefuNaomba kujua jinsi ya kutengeneza dai ya viatu