Kwa vipimo vipi mkuu? Hatuchemshi?
Hii huchemshi mi natengenezaga hivi:
Viini vya yai 4
Mafuta ya kupikia nusu kikombe hadi kikombe kimoja( ukipata olive oil ni bora zaidi
Kitunguu saum kiponde chota kidogo sana
Ndimu kipande 1/vinegar vijiko 3-5
Chumvi
Optionals:-
Flavors nyingine upendazo mfano unaweza ongeza mustard seeds kidogo kiasi robo kijiko cha chai Ila ukiamua kuweka hizi zitwange pamoja na kitunguu thomu.
Pilipili manga ya unga
Vifaa muhimu:
Bakuli
Kikombe chenye mdomo unaweza tumia cha kawaida pia
Uma wa plastic (huu Ni mzuri zaidi unapiga kwa wepesi na kuchanganya bila kelele) Ila unaweza tumia hata wa kawaida
Hatua:
Vunja yai moja moja tenganisha ute na viini
Chukua uma wako anza kupiga mayai kama kawaida, tia chumvi...piga.
yakishachanganyika vizuri chukua kikombe chenye mafuta anza kunyunyizia kidogo kidogo yatoke mfano wa uzi vile huku ukiendelea na shughuli ya upigaji mayai.
Endelea kupiga huku unanyunyizia mafuta Hadi uone mchanganyiko wako unakua na thick creamy texture, (ute mzito)
Stop kumimina mafuta ukiona umepata mchanganyiko unaopendeza,
Anza kuongeza viambata vingine huku ukiendelea kuchanganya vizuri, vinegar, ndimu, kitunguu thomu, pilipili manga.
Hifadhi kwenye chombo chenye mfuniko tayari kwa matumizi.