DOKEZO Wale wa mkopo ESS usijichanganye kuchukua mkopo Azania benki

DOKEZO Wale wa mkopo ESS usijichanganye kuchukua mkopo Azania benki

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Ahead

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2013
Posts
2,410
Reaction score
2,734
Hii benki imenirudisha enzi za ujima na analogy tulipokuwa tunasubiri mkopo wiki mbili mpaka tatu,yaani naenda siku ya tano, kila sehemu umetishwa na makato yameingizwa ila wao hawataki kunipa hela, watumishi wenzangu siku hizi mkopo unaweza kupata hata ndani ya masaa manne ilimradi wapitishaji wawepo online.

Ni wazi hawa azania hawana hela, nikiwapigia wanasema mfumo unashida, lakini si kweli maana benki zingine zinaendelea kutoa, nilitaka ku cancel nichukue benki nyingine wanasema hawana access na mfumo,kifuatacho tutaelewana tu.
 
Tunaweka bwashee wala hatuna haraka na pesa zetu mangi
Hapo lazima shida itakuwa ni mfumo. Hali kama hiyo iliwahi kumtokea mtu na alipopiga simu kuulizia, akaambiwa kuna changamoto ya kimfumo ambapo mfumo wa bank ulikuwa hauna link na mfumo wa ess. Hivyo wakitoa mkopo hawatokuwa na records sahihi za mikopo iliyotolewa. Hivyo mtoa mada avumilie tu, mfumo ukikaa sawa atapata.
 
Hii benki imenirudisha enzi za ujima na analogy tulipokuwa tunasubiri mkopo wiki mbili mpaka tatu,yaani naenda siku ya tano,kila sehemu umetishwa na makato yameingizwa ila wao hawataki kunipa hela,watumishi wenzangu siku hizi mkopo unaweza kupata hata ndani ya masaa manne ilimradi wapitishaji wawepo online.
Ni wazi hawa azania hawana hela,nikiwapigia wanasema mfumo unashida, lakini si kweli maana benki zingine zinaendelea kutoa,nilitaka ku cancel nichukue benki nyingine wanasema hawna access na mfumo,kifuata.....tutaelewana tu.
Wewe bado upo kwenye dimbwi la umaskini na umeshakuwa addicted na mikopo. Sio Kila tatizo linatatuliwa na mikopo weka akiba mnyampaa utakuwa mtumwa wa mabenki na vi microfinance
 
Hapo lazima shida itakuwa ni mfumo. Hali kama hiyo iliwahi kumtokea mtu na alipopiga simu kuulizia, akaambiwa kuna changamoto ya kimfumo ambapo mfumo wa bank ulikuwa hauna link na mfumo wa ess. Hivyo wakitoa mkopo hawatokuwa na records sahihi za mikopo iliyotolewa. Hivyo mtoa mada avumilie tu, mfumo ukikaa sawa atapata.
Hii ni mbaya sana shindii 🥲 umefafanua kwa kirefu mno
 
Mkuu pole sana kwa changamoto hii lakini nukuondoe hofu , Azania ni banki sahihi kwa kila kitu ukilinganisha na mabenki mengine. Eendelea kuwasiliana nao kwa ukaribu itakuwa shida ya mfumo tu. Ni juzi ti hapo nimeupopoa mkopo kwao within 12 hrs. Wako vizuri mmno hawana mbamba hata kama mamitandao ya simu yanakudai .
 
Waaambie umeghairi ili waufute ukakope kwingine,,ukiacha riba kubwa NMB wapo smart sana,,mkopo ndani ya dakika 5
 
Waliounda mfumo kwa nini hawakuweka sehemu ya malalamiko/maulizo (enquires)...!???
 
Bado haipo sababu ya wewe kuhamasisha watu wasikope AZANIA.

madhila uliyokumbana nayo hayalingan na hasara unayotaka waipate
 
Back
Top Bottom