Wale wa saint Kayumba mnakumbuka nini?

Wale wa saint Kayumba mnakumbuka nini?

Duuu kiatu jamani nilikuwa nanunuliwa kiatu kikubwa hatari mbele ni kunawekwa matambara ili kinitoshee yaan cha shule hicho hicho cha kanisan,siwez kusahau nimebeba sana mifuko almaarufu Marlboro,..ahaaa ebwana enz hizo kwenu mkiwa tu na TV mpaka shule unaheshimiwa na wenzako tuliita video,bado nakumbuka tulikuwa na tabia ya kuvaa ndala siku ya kufunga shule na kama una mtu ulikuwa na bifu naye basi unafunga naye shule yaan mnapigana njiani!... Hahaaaa siwez kusahau nilikuwa nauza keki za mwl darasan darajambili shule ya msingi Arusha, jamani nilikuwa navaa mauniform oversize ukilalamika unaambiwa utakuwa nazo ...
 
Mwlm mmoja aliitwa Mwlm Muro Darajambili Arusha sasa ni mchungaj ebana eee kichapo chake kilikuwa heavy,mi nilikuwa na tabia nikimuona Mwlm mtaani namuita kwa nguvu halafu akigeuka tu najificha maana chocho za Ungalimited Arusha zilikuwa n hatar yaan hiyo ilikuwa hobi kwangu duu siku moja kidogo nishikwe ila mtt wa ngaleloo bongonyoo enzi hizo kushikwa sio rahisi chocho nilizijua kama nn ukiniona sasa hiv huwez kuamin
 
hiyo ya kujificha kwenye bendi aisee!nilijifunza kupiga filimbi bila kupenda
 
tulikuwa tunawapa majina walimu,mmoja alikuwa mfupi tukamwita kipipa....mwingine alikuwa anavaa kikoti cheusi kina mistari ya brown kinafanana na aina ya panya fulani huku kwetu dodoma tunawaita nyagala na alikuwa habadilishi!tukampa jina la mwl nyagala.
 
Back
Top Bottom