Wale wa Songea, tufahamiane na kukumbushana mawili matatu

Wale wa Songea, tufahamiane na kukumbushana mawili matatu

Ahee narudi nyumbani ooh...
Ahee narudi Songea oho
Nakwenda kutekeleza agizo la nguvu kazi.Nakwenda kushirikiana na wazee.
Nyumbani ni nyumbani hata kama ni kubaya.Mama ni mama hana mfano.Kwa baba yako ni kwako...

Ahee narudi Songea ohoo
Nakwenda kula likolo linanyungu.Wangoni wote muyumuke mwavalongo wangu...
Ahee narudi Matimila...

Daa!Zamani ilikuwa raha.Ukanda huu wa Songea hadi ziwani(Nyasa)umebarikiwa sana.Kuna wakati Ruvuma ilikuwa tegemeo la nchi kwa chakula.Nenda ziwani.Utakutana na samaki watamu kuwahi kutokea duniani lakini watu walio wengi hawajui kwasababu aina ya uvuvi bado ni ya kizamani ambapo samaki wanavuliwa kwa uchache tu.
Nenda kwenye burudani!Mganda,kitoto,chioda(kioda),ligambusi nk.Leo hii watu wangeweza kutajirika kupitia ngoma ya mganda tu kama juhudi fulani fulani zingefanyika.(Kumbuka Makhirikhiri walikuja wakapiga pesa wakasepa).Kwa maoni yangu mganda huko juu zaidi.
Any way mambo ni mengi...ngoja uzi uendelee kwanza nitarudi baadaye...
 
usengwile wanachama usengwile wa songea alela kumanya aeeeeee alela kumanya aeeeee.....
 
Songea mkoa kero kwa maendeleo ......umnachimba lami unafukia udongo.....barabara ya lami moja tuuuu...,......aisee chalii yangu songea mkoa Wa mazoea.....haaa...haaa....idadi ya bodaboda na watu ni sawa .......sasa basi tutoto tudogo tuna watoto.....afadhari ya kwetu singida bhana......naikumbuka kwa hudumu Fulani Fulani niliyopata ....mpechi....holiday Inn....mtei gesti house.....lamshaba....tulivu .....Jordan gest
 
Liti Madaba. Nakumbuka timu ya mpira ilikuwa hatari sana namkumbuka Computer. Uuwanja Wa Madaba ipale center. Kwa Wandendeule .. Kipindi hicho mkienda Songea town njiani ukimkuta mtu na gari yake imepata pancha mnamuambia vipi Rambo unalalamika pancha wakati kuna Oko !
ulikuwa liti kipindi kipi mkuu?.. mwingira, kombe, nkenwa, ama kisinga?
 
Daaah mkuu kumbe we mboy

Tamsala vp ulienda Pin, na Joint Mass vipi Milango 9, bustani, kuchunga ng'ombe, shadufu, Mashineni

Hahahaha, ukitaka kujua mboys lazima ataje hivyo vitu! Umenikumbusha mbali sana kuhusu Tamsala...
 
Ila songea boys ya wakati ule ....ilikuwa kiboko ....wazee Wa kwenda disco tamsala .....na chupa ya ulanzi
 
Wakuu Salam kwenu.
Wale wa Songea , Songea yetu ya wangoni, wamatengo, wayao na wengine wengi, wale tunaopita njombe, Lilondo, madaba, mkongotema, shule ya Tanga, mbinga, Nyasa, mbambabay, lituhi, matimila njooni tusemezane kitu wanalizombe
Mfaranyaki Bombambili Matomondo Mwembe chai Gerezani Mpamba Lyoto,Nationa Milling Majengo B National Housing japo mm sio wa huko but nina idea na huo mkoa
 
Kuna mchoraji mmoja wa zamani kinyama anaitwa bymchaka sijui kama bado yupo na mpiga picha wa zamani zakuminya.....long long time
 
Bila kusahau ni washirikina sana,mkoa hauna kiwanda hata kimoja.wakunyumba hoyeeeee!!!??
 
Mbona hamtupi vitu vya kiuwekezaji kiuchumi, viwanda, hotel na mambo mengine!!! Naona mnataja majina ya mitaa na vijiji .. Basi wekeni hata picha tuone mkoa ulivyoendelea
 
Liti Madaba. Nakumbuka timu ya mpira ilikuwa hatari sana namkumbuka Computer. Uuwanja Wa Madaba ipale center. Kwa Wandendeule .. Kipindi hicho mkienda Songea town njiani ukimkuta mtu na gari yake imepata pancha mnamuambia vipi Rambo unalalamika pancha wakati kuna Oko !

Mechi kal ilkua ni kati ya Daban(Madaba) vs Njegea. mechi iyo ilkua lazma ngumi zipigwe, ugomv huo uliendelea adi kwa madogo wa primary wakikutana madab na njegea ilkua lazma watandikane manati
 
Back
Top Bottom