Wale wagumu wa kupiga simu tukutane hapa

Wale wagumu wa kupiga simu tukutane hapa

Mi nakata hadi miezi miwili mzee namtumiaga hela bank kwahyo huwa hatuwasiliani labda kama kuna kitu flani
 
Wewe ni kama mimi asee mi kuna muda adi najishtukia😁😁
Mimi sio kupiga tu hata kupokea sipokei simu za watu na hata sijui ni kwanini, ndugu wote walishanisusa kunipigia simu, hata mtu akiwa na shida anampigia wife aniambie, hata sijui tatizo ni nini?
 
Ukweli nimefarijika sana kwamba huu ni udhaifu wa wengi, yani huwa inafika wakati nammisi bimkubwa, nawamiss sana ndugu zangu ila siwapigii simu. Sijui nifanye nini kubadili hii hali
 
Ukweli nimefarijika sana kwamba huu ni udhaifu wa wengi, yani huwa inafika wakati nammisi bimkubwa, nawamiss sana ndugu zangu ila siwapigii simu. Sijui nifanye nini kubadili hii hali
Na kunawakati unataka hadi kupiga unawaza namwambiaje yaan nilikuwa nakusalimia tu
 
Mwenyewe na kauvivu flani kupiga cm hata sms kumtafuta huwa nasemaga ngoja nitamtafuta Kesho au baadae hapo ndio imetoka...Lkn ikitokea mtu kanipigia au katum sms nakuaga na story nyingi yaani Hadi anasahau kama simtafuteg
Wewe ni kama mimi mkuu. Hii hali naichukia sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tupo wengi Mkuu. Kila Mamamkwe anaponipigia simu lazima nitumie dakika tatu mpaka tano naomba msamaha kwa kutompigia simu na kuahidi kujirekebisha. Lakini bado niko vilevile. Wiki ya tatu sasa, rafiki yangu wa damu wa utotoni kapata ajali ya gari na kulazwa hospitali huko Dar. Sijawahi hata kumpigia simu wakati vocha ninayo. Nasoma tu tarifa zake kwenye group letu la WhatsApp!
Mpigie. Wewe ni wakuwekwa makofi mpaka uzirai maana umezidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wife analamika ila supend kuongea na wewe coz hakuna cha kushare
 
Ila wazazi wengi naona wanapenda Sana hizi mambo za kupigiwa pigiwa simu mara kwa mara, eti wao wanaona ndo heshima na kuwapenda, mi nimeshaparuana na ndg wengi ajili ya hii kitu lakn bado nimekuwa vilevile, tena wanapoharibu ni wanapoanza kunung'unika na ishu hizi ndo kabisaaa mudi inapotea hapo ndipo sitaipiga simu kwa muda mrefu sana,
 
Huwa sipendi ongea na watu, ila kazi yangu inanilazimu kuongea na mzee 1 karibu kila siku na huwa ananipigia mara nyingi ila nakuwa mvivu kupokea (yeye huwa ananiambia niachie kuweka silence kumbe ni vile naona(ga) shida kupokea


Napenda meseji zaidi kuliko kuongea, kwa ndugu wao ndo hunipigia tofauti na hapo tutakaa hata miaka 2 kimya
Hata mim napenda sms zaidi, kwani mtu anakuwa straight kwa points kuliko maneno mengi ya kulaumiana.
 
Kuna siku nilipokea mzigo usiku wakati nilitakiwa kupata mchana kisa tu siku piga Simu kujua mwenendo wa basi itakua iko pande zipi nilichelewa kupiga Simu mama kanionya wee yani adi a nitafute
 
Kweli hii kitu hutokea nilijua nipo peke yangu,kumbe tupo wengi.Kila nikusema nianze kubadilika narudi kule kule
 
Hii inawezekana ni tabia ya introverts. Na nimegundua pia kwamba JF wengi ni Introverts.

Mi nakumbuka mwaka 2015 maza alinipigia simu kunilalamikia kwamba simpigii simu.. na hapo ni kweli nimeshakaa zaidi ya miezi miwili hatujawasiliana kwa simu.

Mwenyewe kipindi hicho nilikuwa nimevurugwa na maisha, nikaona huyu maza ananizingua na huku kulalamika, ikabidi nimuambie, 'Ukiona sikupigii, uwe unanipigia wewe'... Tangu wakati huo hajawahi kulalamika tena.

Na mtu akinilalamikia kwamba simpigii, ndo sitampigia tena. Kuna rafiki yangu mmoja huwa ananijua, yeye huwa tunawasiliana kwa mwaka mara tano..
 
Hata mimi hili tatizo ninalo, ngoja nianze kujirekebisha, lkn haya yote yanachangiwa na kuwa na hizi smart phone, tuko bize sana kwenye internet.naamini tungekuwa na simu tochi tungekuwa tunapigiana

Hata ununue simu za vitochi 100 utembee nazo ila utashindwa tu kupiga simu sababu ni hulka hiyo.
 
Mimi hili suala linanitatiza kwa sasa....sina mazoea na mshua....hajanilea kwa kunijengea urafiki na yeye. Mpaka nimefika utu uzima mimi na mshua hatunaga stori kabisa.

Naweza kukaa 2 months sijampigia simu..na yeye hajanipigia pia na nikawa comfortable kabisa.
 
Tupo wengi mkuu, mimi huwa napanga kupiga simu kama vile napanga safari ya kwenda Zanzibar, nikimaliza kupiga (nikizidi dk 3 basi hayo ni maongezi marefu) huwa najihisi kama nilikuwa nimebeba mzigo mzito sana na sasa nimeutua...! Wakati mwingine huwa naona bora niende nikamsalimie mtu kuliko kumpigia simu!
 
Back
Top Bottom