Wale waliotoweka na kapu la sadaka pale Ufufuo na uzima, ndio hao wanaochunguza fuko la pesa za mchina?

Wale waliotoweka na kapu la sadaka pale Ufufuo na uzima, ndio hao wanaochunguza fuko la pesa za mchina?

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
25,937
Reaction score
41,161
Salaam!

Walipofunga utepe kanisa la Ufufuo na uzima,palikuwa na sadaka kwenye kapu, palikuwa na mali mbalimbali,walipovamia na kutawanya watu Kisha kuweka utepe, kulikuwa shwari kabisa.

Kinachochanganya Hadi sasa,haijulikani kapu la sadaka walipeleka wapi Hadi Leo, Pana upotevu mkubwa wa mali za kanisa, na hawataki kuhojiwa chochote.

Leo imeripotiwa watu wale wale wamevamia nyumba ya mchina na kumkuta na kiasi kikubwa Cha pesa, na wamezichukua kwenda kuzichunguza, narudia msisitizo ni "kuzichunguza pesa za mchina"!

Swali: Waliopotea na sadaka pale Ufufuo na uzima na Hawa wanaochunguza fuko la pesa za mchina ni kutoka nchi ya Malawi au ni wale wale?

Karibuni!
 
Bahati mbaya wachina hawajui kiswahili
Wataibiwa mchana kweupe
 
Bahati mbaya wachina hawajui kiswahili
Wataibiwa mchana kweupe
Hata kama ni pesa haramu,

Je Hawa waliozishika pesa hizo Wana maadili ya kutosha kuchunguza pesa nyingi kiasi hicho na zikabaki salama?

Ni Hawa wanaoishi kwenye mabanda ya mabati full suit?
 
Back
Top Bottom