Wale walokataza waumini wao kutopokea zawadi wala kula ubwabwa wa krisimasi

Wale walokataza waumini wao kutopokea zawadi wala kula ubwabwa wa krisimasi

Wale ambao hawakuisoma vzr dini na historia yake ndio waliojaa na kujifanya wafia dini ma viongozi wanaolisha watu ujinga hususani Africa
 
Nimekutana na kijana wa kiislam akilalama kuwa wakristo wameshusha vitu vizito sikukuu hii ya mwaka mpya huku wao waislam hawana shamrashamra na maakuli, anashangaa kwa nini wao waislam wanaipotezea tena hii sikukuu ya mwaka mpya? Waislam wana matrix nyingi sana wanahitaji kukombolewa fikra zao
 
Ngoja tuende darasani kidogo wanajf,yanayo pingwa ni mambo ya kiibada,ibada ni matendo ya kiimani ambayo wasio waislamu huyafanya kwa mujibu wa imani zao,kama hayo ya kuamini Mungu/Yesu alizaliwa Dec 25,hatuna shida na imani yenu

Kwetu sisi kushiriki ibada za kishirikina na kikafiri ni haramu,maana nasi tukisheherekea sikukuu hiyo ni kana kwamba nasi tunaungana nanyi kwenye imani yenu

Na jambo lolote katika uislamu linahukumiwa na nia au makusudio ya mtu husika,mfano kuletewa chakula kama chakula nikiwa nyumbani kwangu hakuna ubaya,huo ni ujirani mwema,ingawa kwa baadhi ya waislamu wanaona haifai,hiyo itabaki ni mtazamo na imani ya mtu binafsi

Uislamu unahimiza juu ya umuhimu wa kuishi vizuri na majirani,kwahiyo kitendo cha kupewa chakula na jirani ni jambo zuri,maadamu sikuweka kusudio la kwenda nyumbani kwake kusheherekea ibada yake.

Haya mengine mnayoleta hapa ni mawazo yenu binafsi na mnajifurahisha nafsi zenu kama kawaida yenu


Asante
 
Watu wa dini mzinguaga sana badala mpendane nyie mnachukiana tena wazi wazi

anyway kwasasa tuachie nguvu ya harufu ya pilau ifanye kazi!

Happy nu yeaa 2026.
 
Back
Top Bottom