Wale Wanaopanga kumiliki magari used ya bei Nafuu: Tazama plan Yetu bila Riba

Wale Wanaopanga kumiliki magari used ya bei Nafuu: Tazama plan Yetu bila Riba

Dr. Zaganza

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2014
Posts
1,814
Reaction score
2,738
Habari zenu wakuu.
Baada ya kukutana na vijana kadhaa wanatamani wamiliki gari used kuwahi shughuli zao ila bajeti haitoshi, Yaani ni kazi kukusanya milioni 5 au 4 kwa pamoja.
Naielewa vyema hali hiyo nami nilipitia nikianza maisha ya kujitafuta. Sasa nimekuja na plan kuwawezesha kutimiza malengo yenu bila Riba.
Tumeanzisha utaratibu wa kukusanya watu kati ya 4 hadi 8 kwa kikundi, kila mmoja akiwa na mtaji usiopungua laki 5 na usiozidi milioni moja. Vijana hawa watasajili kikundi chao BRELA na kwa mwanasheria. Milioni 5 au 4 watalipia gari moja used na kupanga utaratibu wa kulitumia gari lao.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa 0713-039 875
Tuko Kibaha maili moja



WhatsApp Image 2025-08-07 at 12.03.35.jpeg
WhatsApp Image 2025-08-07 at 12.03.34.jpeg
 
Vijana hawa watasajili kikundi chao BRELA na kwa mwanasheria. Milioni 5 au 4 watalipia gari moja used na kupanga utaratibu wa kulitumia gari lao.
Hapo unakuwa umewasaidiaje vijana?
 
Hii inaitwa ujamaa .

Hatua ya pili tunanunua ekari ya ardhi na kugawana mita 20 kwa 20 kila mmoja
 
Fikiria vijana wanne wanaokaa kimara na kazi posta

Pia fikiria misuli yao ya kiuchumi ni ya wastani

Hapo plan yetu ni mkombozi wao
 
Habari zenu wakuu.
Baada ya kukutana na vijana kadhaa wanatamani wamiliki gari used kuwahi shughuli zao ila bajeti haitoshi, Yaani ni kazi kukusanya milioni 5 au 4 kwa pamoja.
Naielewa vyema hali hiyo nami nilipitia nikianza maisha ya kujitafuta. Sasa nimekuja na plan kuwawezesha kutimiza malengo yenu bila Riba.
Tumeanzisha utaratibu wa kukusanya watu kati ya 4 hadi 8 kwa kikundi, kila mmoja akiwa na mtaji usiopungua laki 5 na usiozidi milioni moja. Vijana hawa watasajili kikundi chao BRELA na kwa mwanasheria. Milioni 5 au 4 watalipia gari moja used na kupanga utaratibu wa kulitumia gari lao.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa 0713-039 875
Tuko Kibaha maili moja



View attachment 3434766View attachment 3434768
Kuna vitu hautakiwi kulazimisha kumiliki, mfuko ndio unaotakiwa kukulazimisha.Ninajua washkaji zaidi ya watano walinunua magari yao ya kwanza kipindi cha mvua Dar es salaam. Walikuwa na hela lakini hawakuona umuhimu mpaka barabara zilipojaa matope na hata wakitumia boda boda wanachafua suruali zao.
 
aisee yaan nishare chumba na mkewangu bafo nikashare magari na watuu

uwiiiiiii labda tununue

ambulance
 
Pia kingine kwenye plan yetu kuna chaguo la kupewa dereva wa kujitolea kwa mwezi mmoja endapo bado wanampango wanashughulikia leseni au wanajifunza kuzoea City center
 
Kwa uzoefu wangu wa ziara baadhi ya nchi, vitu kama gari na nyumba ni vya kulipa kwa awamu . Ni njia pia ya kuacha pesa nyingi kwenye mzunguko. Chukulia nyumba ya milioni 30 hadi 50 ujenge au kununua kwa cash. Mara idadi ya wastaafu elf moja kwa mkoa mmoja.
 
Unawasaidia kwa kuwapa collateral badala ya asset ? Hilo gari litakuwa linaingiza kiasi gani zaidi ya kuwatoboa mifuko kwa kununua wese na eventually kuharibika / kuwa scrapper ?

Katika Maisha anza kwanza kwa kununua rasilimali inayokuingizia kipato / ukishapata basi ndio ununue hizo wants nyingine..., (live within your means)

Wazo lako badilisha kawasaidia wakulima kununua tractors
 
Gari ni kwa matumizi binafsi ama biashara kama uber,bolt n.k .kuna wazazi wanapenda school bus ndogo ibebe watoto wachache, chaguo ni lenu
 
Hivi Kweli dokta umeumiza kichwa Kwa kutumia elimu yako hili ndio wazo umeona uje nalo? Au hii doctorate ni kama ile ya Dr musukuma, au Dr Babu tale?
Hata msukuma darasa la saba ila anaitwa Dokta.
 
Inakuwaje pale wana group mmoja anaishi Kimara, Mwingine Chanika, kuna wa Mbweni na wa mwisho maji matitu.

Wata share vipi gari?
 
Jikiteni kwenye mada wakuu ndo heshima ya jf.
Usitaje asiyehusika . Msiingie mkumbo wa wale wanaosimanga marehemu na kabla hajafa hajamsema.
 
Inakuwaje pale wana group mmoja anaishi Kimara, Mwingine Chanika, kuna wa Mbweni na wa mwisho maji matitu.

Wata share vipi gari?
Swali zuri. Ni Kama school bus, woote watapitiwa ,wa mbali mapema zaidi mfano saa 11 n.k .pia kwa baadaye kutakuwa na vituo unatumia gari mojawapo ya plan yetu iliyo jirani nawe
 
Back
Top Bottom