Wale wapenzi wa Perfume/Body Spray, tukutane hapa

Blue 4Men,25,000/= tu inadumu kwenye nguo zaidi ya masaa 24 ni vile sirudii nguo navaa mara moja but nahisi inaweza kusogea zaidi ya hapo.

Mwaka wa kumi na sita huu naitumia but nilishawahi kujaribu kuibadilisha ila sijapata mbadala wake,kingine ajabu ya perfumes anaweza kutumia aina hii mwenzako ukaisikia harufu yake ilivyo nzuri then aina hiyo hiyo ukaitumia wewe ukahisi harufu tofauti kabisa.
 
Hii ni kweli.. Kuna harufu moja ya perfume jamaa wangu alikuwa akipenda kutumia kupaka, ilikua inakera kichizi.
Yani nikimsogelea karibu ni lazima nipige chafya za kutosha.
Nikatokea kuichukia tu, lakini yeye anaikubali hatari!
Nimeisahau jina.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…