Wale wapigaji wa maji au vyombo tukutane hapa

Wale wapigaji wa maji au vyombo tukutane hapa

cheetah255

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2017
Posts
1,376
Reaction score
2,393
Kuna aina nyingi za vinywaji vya kulewesha wengi tumekua tukijiburudisha na vinywaji hivyo baada ya kutoka kazini au tukiwa tumepumzika nitachambua baadhi kwa uzoefu wangu.
Aina ya kwanza ni
Beer▶kuna za kisasa kamavile tusker,Safari,Kilimanjaro,Balimi,plisner,Kibo na za kienyeji kama chibuku na mbege hizi zote hulewesha taratibu unapotumia na endapo utatumia kwa muda mrefu utapata hadi kitambi.

Dry gin▶Hii ni aina nyingine ya pombe zipo za kisasa kama Konyagi,Kvant,London dry gin,Gordons ,Consulate n.k pia kuna zakienyeji kama Gongo na babilong aina hizi za dry gin zinalewesha haraka tena kwa kutumia kiasi kidogo tu kama utapendelea kutumia aina hii ya pombe lazima uwe umekula vizuri nyama au mapafu ya ng'ombe na unapotumia drygin ni muhimu uwe na kipande chalimao utakata kipande na kudumbukiza kwenye glass endapo hauta fanya ivyo utasumbuliwa sana na hangover.

Vodka▶Hii ni aina nyingine kabisa ya pombe ni vilevi kama magicmoment,Ciroc,Smirnoff,Gallaxy,Skyblue n.k aina hii ya pombe huwa na ladha pamoja na harufu tofauti kama vile taste ya chungwa,chocolate,nanasi na kahawa hizipombe huongeza hamu ya kufanya tendo la ndoa sana mfano pale mwanamke atakapo tumia magic moment na mwanaume atumie campari.

Whisky▶Kuna aina nyingi za whisky kama grants,jack daniels,Redlabel,Hennessy n.k aina hii ya pombe inatakiwa ikae kwa muda wa miaka angalau mitano na kuendelea ili iwe na kilevi murua pamoja na ladha nzuri kuna utaratibu wa kunywa aina hii ya pombe unatakiwa unywe kimafundo mafundo usinywe kama chai endapo utakunya kama chai hii pombe ina tabia ya kuunguza sana mdomo na kubabua lip

Brandy▶hii nia aine nyingine ya pombe kama vile value,hennessy x.o,n.k aina hizi zapombe huwa tamu tamu na zinalewesha haraka pia hulainisha viungo vya mwili kama magoti na mikono hizi pombe huwa zina muacha mtumiaji na kiwango kikubwa cha hangover akiamka.

Wine▶hii ni aina ingine ya pombe nitamu sana misili ya soda na maranyingi huwa hazileweshi sana mfano wa wine ni kama dodoma wine,Dompo,Robertson wine n.k nb kwa mnywaji mzuri wa pombe akinunua wine anaona kama kapoteza ela bure.

RUM▶hizi ndyo pombe adimu duniani na ghali sana mfano wa hizi pombe ni Pelican western rum na Hennessy extra odinary ndiyo pombe pekee niliyo wahi kunywa na sikupata hangover ata kidogo. Karibuni tubadilishane uzoefu wa kupiga vyombo.
 
554a51aee38bb6238f995ab5148b42c3.jpg



Njoo happy hour hapa new africa tupige vyombo sasa
 
Mi nakulaga Balimi ndogo kuanzia chupa 10 hivi nachanganya na valuu viroba vitano ndo akili inakaa sawa nikiamka asubuhi nawahi supu ya nguvu ya mbuzi na ndizi za kuchemsha,
Napendaga zaidi Balimi na Valuu na sometimes Grant's
Cheers[emoji482] [emoji482] [emoji482]
 
Mi nakulaga Balimi ndogo kuanzia chupa 10 hivi nachanganya na valuu viroba vitano ndo akili inakaa sawa nikiamka asubuhi nawahi supu ya nguvu ya mbuzi na ndizi za kuchemsha,
Napendaga zaidi Balimi na Valuu na sometimes Grant's
Cheers[emoji482] [emoji482] [emoji482]
Cheers mkuu ila value ukiongeza na sigara kali kichwa si kitapasuka?
 
Hakuna kama KONYAGI..
Kunywa
Ongeza
Nyege
Yako
Angalia
Gongo
Itakuua
Hii ndio maana halisi ya KONYAGI...
 
Back
Top Bottom