Mtambachuo
JF-Expert Member
- May 6, 2023
- 1,907
- 3,560
- Thread starter
-
- #41
Wewe degree yako ni yakusifia sifia kama Mwijaku huna lolote, nje ya kuajiriwa wenye degree ni takataka tuu.Watu wengi ambao hawana degree huwa wana wasiwasi sana... kamwe msomi hawezi kuwa sawa na asiyesoma. Kwenye suala la hela msomi ana nafasi nyingi zaidi ya kupata kuliko mtu wa darasa la 7. Na wengi ambao hawana degree wana maisha magumu kulinganisha na wenye degree.
Naendelea kupambana na maisha mkuu. Salamu kwako.Tuko poa sana, vipi upande wako mkuu?
Pambana ukifika mtaani utakuja kukomenti vizuri.Sisi Third Year wa BSc tunakomenti wapiii?
Hata mtaani kazi za wakala, maduka n.k degree holders na diploma zipo za kutosha ila ukitafakar kwa mapana utaona kwamba hata wao wangeweza kufungua biashara kama hizo, sasa sijui ni uoga au ni nini.Wewe degree yako ni yakusifia sifia kama Mwijaku huna lolote, nje ya kuajiriwa wenye degree ni hawana lolote.
Hao daraa la saba unao wabaganza hapa ndio wenye biashara kubwa huko kariakoo na kwingine na wamewaajiri nyie na hizo degree zenu.
Mawazo mazuri mkuu hongera sana unafaa kutunukiwa Shahada ya Udaktari wa heshima katika biashara.Mimi nasema haya kutokana na ushuhuda wangu binafsi.
Wakuu, kama umesoma level ya diploma, degree na kuendelea na hauna kazi, yaani hujaajiriwa. Jaribu kupambana na kabiashara chochote kale au hata kakikazi ambacho kanafanywa na watu ambao ni std 7 au form 4 leaver, ukikifanya wewe mwenye elimu yako utakifanya ktk utofauti mkubwa na hapo utapiga ela, utavuta wateja kwa wingi.
Mimi kuna muda niliamua kuachana na ajira ya laki 6 na nikaamua kujiajiri mwenyewe. Mambo yangu sio haba sababu napata muda mwingi wa kufanya mambo yangu na napata utulivu mkubwa sana ktk maisha yangu tofauti na nilivyoajiriwa.
Naweka balance ambayo sikuwahi kuwa nayo nikiwa ktk ajira. Kikubwa nnachotaka kusema kwa graduates, usidharau kazi yeyote ile, anza kuifanya, weka strategies nzuri za kibiashara, ipende hiyo kazi. Kama ni mwanaume jaribu kujiweka mbali na anasa za wanawake unless uwe na mmoja ambae hana mambo mengi, jitahidi sana kuipenda na kujituma ktk hiyo kazi, Mungu atakusaidia utafanikiwa tu.
Tunakula Maisha tu,wewe je?Wana jamvi kwema,
Leo nimeona niwajulie hali hawa ndugu zetu wenye BSc na BA na degree nyinginezo, vipi maisha yanaendaje baada ya kuhudhurishwa na kutunukiwa Shahada yako.
Vipi mategemeo uliyokuwa nayo, yame kuwa sawa na uhalisia huko duniani? Je, kati ya BSc na BA ipi imesaidia angalau kwenye kujikwamua nje ya ajira, yaani kujiajiri au kutumia ujuzi wako uliopata kutatua changamoto mbalimbali za maisha?
Asamaleko.
Kushindwa kwako kutambua uhusiano mdogo sana uliopo kati ya IQ na pesa ndo kunadhihirisha umuhimu wa kuwa na elimu.IQ kubwa mtu analala njaa hana hata akiba benk kazi kuomba 1000. Hiyo IQ imasaidia nini.?
Wangapi wenye hizo biashara kubwa?wako wapi hao? Mbona huku Uraiani hawaonekani 😀Wewe degree yako ni yakusifia sifia kama Mwijaku huna lolote, nje ya kuajiriwa wenye degree ni takataka tuu.
Hao darasa la saba unao wabagaza hapa ndio wenye biashara kubwa huko kariakoo na kwingineko na wame waajiri nyie na hizo degree zenu.
Wengi wana uoga wa kushindwa hilo ndio tatizo, kila kitu anataka atumie elimu ya darasani na hawapendi kupokea ushauri kwa wazoefu kisa hawana diploma au degreeHata mtaani kazi za wakala, maduka n.k degree holders na diploma zipo za kutosha ila ukitafakar kwa mapana utaona kwamba hata wao wangeweza kufungua biashara kama hizo, sasa sijui ni uoga au ni nini.
Mkuu mimi nilianza biashara napata faida laki per month, hapo nimetoka ktk ajira ambayo nilikuwa napokea at least 600k per month.
Namshukuru Mungu kwa sasa najiona kule kwenye ajira nilikuwa nimepoteza sana muda.
All in all, sote tunaamini kuna majira pia ambayo Mungu huwa humuinua mtu.
Wapo kibao wewe leta tafiti yako ya kuonesha kuwa hawapo.Wangapi wenye hizo biashara kubwa?wako wapi hao? Mbona huku Uraiani hawaonekani 😀
Hii misemo yenu muwe mnaifanyia utafiti kwanza
Nina rafiki yangu kuna siku nilipishana nae anauza mikanda, nilishtuka sana mkuu. Huyu jamaa nilisoma nae chuo, sasa kuna siku akanipigia simu ananiomba ushauri amepata kazi sehemu mbili, moja mshahara laki 2 kamil na hakuna nauli na ya pili alipwe 150,000 ila mshahara ni elfu mbili sijui tano kwa siku na ofisi iko mbali.Mawazo mazuri mkuu hongera sana unafaa kutunukiwa Shahada ya Udaktari wa heshima katika biashara.
Hawaonekani mtaani hao darasa la 7 matajiri wenye mabiashara makubwa makubwa na makampuniWapo kibao wewe leta tafiti yako ya kuonesha kuwa hawapo.
Ndio mkuu kikubwa ni kupambana hata kwa kuanzia chini mwisho wa siku utakua ila ajira ya laki 2 kwa mwanaume mwenyewe majukumu atachelewa sana.Nina rafiki yangu kuna siku nilipishana nae anauza mikanda, nilishtuka sana mkuu. Huyu jamaa nilisoma nae chuo, sasa kuna siku akanipigia simu ananiomba ushauri amepata kazi sehemu mbili, moja mshahara laki 2 kamil na hakuna nauli na ya pili alipwe 150,000 ila mshahara ni elfu mbili sijui tano kwa siku na ofisi iko mbali.
Nilikuwa naongea nae nikiwa nasikitika sana, mbaya zaidi akanambia kuna mwanamke ameamua kuishi nae. Nikajiuliza kwani vijana tunafeli wapi? Kwanini mtu unakomaa na ajira, hiyo laki na nusu au mbili si bora utafute hata bajaji au bodaboda uendeshe after 2 au 3 years yamkini ukawa na chombo chako?
Au laaah ufungue hata kaofisi cha uwakala uwe na line hata 3 tu uanze nazo. Kwanini ukomae tu kuajiriwa ambapo maslahi ni ya chini sana? Jamaa sikutaka kumweleza sababu ingeonekana ni kama namdhihaki, hata ile siku nliyomuona yupo anauza mikanda sikutaka kumshtua na nilimsifu sababu mwanaume unapaswa kupambana haswa ili kupata ela.
Kabisa tuone kwamba ina wezekana nje ya vyeti na ukianza biashara yako hata kama ni ndogo uweke jitihada zako zote hapo na uwe tayari kujifunza na kushirikiana na wengine.Mimi nafikiri wale ambao kidooogo tumeenda shule, embu tuondoe dhana ya vyeti vinatulinda na vitatutoa kimaisha.
Tufanye kwamba hatuna vyeti na tunapaswa tupambane tutoke kimaisha. Tuchakate bongo zetu tutafakari hawa ambao hawana hivyo vyeti mbona wanaishi? Kwanini kwetu hata ela ya kula iwe shida?
Tuamke jamani tuamke.
Yaani uweke pembeni kitu ulichokipambania kwa zaidi ya miaka 16 ya maisha yako? Badala ya kushauri mtu awekeze katika kutafuta njia bora za kuunganisha taaluma na kipaji chake tangu akiwa shule, wewe unaona ni bora asahau kabisa kama alitumia miaka mingi kutafuta alichokipata.Mimi nafikiri wale ambao kidooogo tumeenda shule, embu tuondoe dhana ya vyeti vinatulinda na vitatutoa kimaisha.
Tufanye kwamba hatuna vyeti na tunapaswa tupambane tutoke kimaisha. Tuchakate bongo zetu tutafakari hawa ambao hawana hivyo vyeti mbona wanaishi? Kwanini kwetu hata ela ya kula iwe shida?
Tuamke jamani tuamke.
Tunaendelea kupiga mamilioni ya kodi yako bila jasho wala presha kwa jina la ubadhirifu..vipi na we huko mtaani unaweza fanya ubadhirifu wa mamilioni ya kodi kama huku kwa wenye degree?Wana jamvi kwema,
Leo nimeona niwajulie hali hawa ndugu zetu wenye BSc na BA na degree nyinginezo, vipi maisha yanaendaje baada ya kuhudhurishwa na kutunukiwa Shahada yako.
Vipi mategemeo uliyokuwa nayo, yame kuwa sawa na uhalisia huko duniani? Je, kati ya BSc na BA ipi imesaidia angalau kwenye kujikwamua nje ya ajira, yaani kujiajiri au kutumia ujuzi wako uliopata kutatua changamoto mbalimbali za maisha?
Asamaleko.
Hii ni hatari sisi huku ni waadilifu sana.Tunaendelea kupiga mamilioni ya kodi yako bila jasho wala presha kwa jina la ubadhirifu..vipi na we huko mtaani unaweza fanya ubadhirifu wa mamilioni ya kodi kama huku kwa wenye degree?
Best savage answer so far👏🏾, safi sana mkuu. Huu mtindo wa kudhihaki watu waliosoma na wakakosa kazi naomba uendelee hivi hivi ili kila atakaebahatika kupata nafasi sehemu aibe sana bila huruma.Tunaendelea kupiga mamilioni ya kodi yako bila jasho wala presha kwa jina la ubadhirifu..vipi na we huko mtaani unaweza fanya ubadhirifu wa mamilioni ya kodi kama huku kwa wenye degree?