Wale wote mliofanikiwa kwenye biashara na watafutaji pitieni hapa

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304
Natumaini wote hamjambo? Mimi na marafiki zangu tumeamua kuelimisha vijana wenzetu namna ya kuboresha maisha yao kwa mifano pia kutoka kwa watu ambao wamefankiwa. Kwa kuanzia tutaanza kuelimisha kwa vijana kutoka nchi za Tanzania na Kenya.Pia tutaelimisha jamii kupitia mtandaoni na hapa JF. Nilikuwa naomba kwa wale ambao wamefanikiwa kupitia shighuli zao za biashara au ujasiriamali wanaweza kutupa historia zao na namna walivyofanikiwa kutoka chini hadi kati au juu.Naomba mtutumie kwenda empoweryouth@yahoo.com

Nitatumia mifano yenu kuelimisha jamii ili kujikwamua na umasikini kwa mifano iliyohai ili watu wajifunze kutoka kwenu. Lengo la kufanya hivi ni maamuzi niliyofikia na marafiki kuelimisha jamii hasa vijana kujikwamua na wao wawe watu miongoni mwa watu.Mimi pia nitatoa nondo kali sana kila siku niko naandika mambo mengi ili kuelimisha.

Naomba mnitumie historia zenu katika biashara ikiwemo na vikwazo mlivyopitia kupata mafanikio na ata picha kama mkipenda kwenda kwa empoweryouth@yahoo.com
 
Kufanikiwa unamaanisha nini? Utakimbiza watu maana binadamu hatutosheki. Hata milionea anatafuta bado atakwambia hajafanikiwa. Labda iwe mfanya biashara au mjasiriamali yeyeto anayeishi kwa mapato ya biashara. Wengine biashara zao hazitumiki kwa chochote anategemea mshahara. Vizuri ufafanue nini wakuelezee.
 
namaanisha aliyetoka kwenye hatua fulani kwenda hatua nyingine si lazima awe tajiri.Kuelimisha kupitia mifano hai ni rahisi kueleweka na watu kuona inawezekana kuliko mifano ya kusadikika au kutolea mifano ya mabilionea wa uko marekan
 
Ok umeeleweka ngoja watakuja hapa sasaivi
namaanisha aliyetoka kwenye hatua fulani kwenda hatua nyingine si lazima awe tajiri.Kuelimisha kupitia mifano hai ni rahisi kueleweka na watu kuona inawezekana kuliko mifano ya kusadikika au kutolea mifano ya mabilionea wa uko marekan
 
Ni ngumu sana kuelezea mafanikio. mfano mimi nilifungua genge na mtaji wa 50000 sasa mtaji wangu umefika 98000 kwangu ni mafanikio ,wakati mwingine hiyo 98 ananunua bia au kiatu kwake si mafanikio. Ngoja waje , lakini msije mkawa unataka business idea za watu halafu unapeleka kwenye shindano lilee....
 
mimi ni mjasiriamali ila sijui nieleze hapa ila nshafanya kazi zote kuchimba madini, kilimo, uvuvi wa jongoo bahari na uuzaji wa makombe ya bahari hadi mapezi ya papa....nkisema nieleze hapaa ntaisumbia server ya jf...
 
Ni ngumu sana kuelezea mafanikio. mfano mimi nilifungua genge na mtaji wa 50000 sasa mtaji wangu umefika 98000 kwangu ni mafanikio ,wakati mwingine hiyo 98 ananunua bia au kiatu kwake si mafanikio. Ngoja waje , lakini msije mkawa unataka business idea za watu halafu unapeleka kwenye shindano lilee....

Kufanikiwa unamaanisha nini? Utakimbiza watu maana binadamu hatutosheki. Hata milionea anatafuta bado atakwambia hajafanikiwa. Labda iwe mfanya biashara au mjasiriamali yeyeto anayeishi kwa mapato ya biashara. Wengine biashara zao hazitumiki kwa chochote anategemea mshahara. Vizuri ufafanue nini wakuelezee.

Hayo ndiyo mafanikio yenyewe, ulipokuwa unaanzisha hiyo kazi ulikuwa na mategemeo na malengo,yanapotimia ndiyo mafanikio yenyewe. Mfano ulifungua genge ukaweka nia na juhudi ukijua baada ya miezi mitatu lau utakuwa unaingiza shilingi elfu kumi kwa siku, kweli baada ya miezi miwili unakuwa unapata faida ya shilingi elfu kumi na tano kwa siku...UMEFANIKIWA, unaendelea kuset malengo makubwa kiasi kwa hatua!
 
Mbona maombi ya Money Stunna yanaeleweka au ndo kila kitu mpka mjitie kujua, kama wewe unahs hujafanikiwa Usitume, wanaohs wamefanikiwa watatuma.

Kama watu wapo kila siku kwa kina upako na wengineo wanaeleza mafanikio yao, itakuwa hapa?

Et mnaoji hata mamilionea hawajaridhika, kha! Kwa iyo c mafanikio hayo ya umilionea? Bas hayo ndo mkuu hapa anahtaji.

Stunna amekuwa mmoja ya watu wanaoleta ideas humu tena nzuri, aibe ili? Mbona ka ni idea za biashara zmejaa humu.
 
mimi ni mjasiriamali ila sijui nieleze hapa ila nshafanya kazi zote kuchimba madini, kilimo, uvuvi wa jongoo bahari na uuzaji wa makombe ya bahari hadi mapezi ya papa....nkisema nieleze hapaa ntaisumbia server ya jf...

shusha nondo watu wafaidike!
 
Halafu MONEYstunna nilikuomba maelekezo juu ya biashara ya nguo uganda,kimya mpaka leo.
 
Last edited by a moderator:

nitumie tena msg hapo kati nilikuwa na mambo mengi pamoja na safari.
 
Last edited by a moderator:
Siri ya matajiri/waliofanikiwa hawawezi kukwambia.

si kweli wengi wanasema mengine yako wazi kwenye kimtandao,na biashara zao ziko wazi na kwenye interview wanasema na ukiangalia unaona sawa kabisa
 
Ni ngumu sana kuelezea mafanikio. mfano mimi nilifungua genge na mtaji wa 50000 sasa mtaji wangu umefika 98000 kwangu ni mafanikio ,wakati mwingine hiyo 98 ananunua bia au kiatu kwake si mafanikio. Ngoja waje , lakini msije mkawa unataka business idea za watu halafu unapeleka kwenye shindano lilee....

lengo ni kuelimisha jamii kwa hiyo mifano hai na mtaipata
 
mimi nimefanikiwa kwa maana nilianza na tsh 200 leo nimefikisha tsh 300, nahii imenihangaisha miaka. miwili kuifikisha mia 3
 
Hapo labda ndo tunapopata kigugumizi MALENGO ni kweli biashara tunafanya na malengo tumeweka sasa kuyafikia ndio issue. Pia biashara kuwa active muda wote tatu malengo kufikiwa ukichanganya na vipato vya ajira. Bado tunajifunza mengi ndio nilisema wale tu wanaoitegemea biashara pekee kufikia malengo yao au hata mchango wa biashara ktk kutimiza malengo ya muhusika?
Hayo ndiyo mafanikio yenyewe, ulipokuwa unaanzisha hiyo kazi ulikuwa na mategemeo na malengo,yanapotimia ndiyo mafanikio yenyewe. Mfano ulifungua genge ukaweka nia na juhudi ukijua baada ya miezi mitatu lau utakuwa unaingiza shilingi elfu kumi kwa siku, kweli baada ya miezi miwili unakuwa unapata faida ya shilingi elfu kumi na tano kwa siku...UMEFANIKIWA, unaendelea kuset malengo makubwa kiasi kwa hatua!
 
Mimi ndo nataka anza. Ila inabidi nijitoe mhanga kwanza
 
wewe haujafanikiwa bado?
bado kwakweli hadi mwaka mmoja niitegemee biashara tu ndipo nitajua hiki kimetokana biashara pekee sio ajira. Mswahili na kutunza hesabu ngumu account zimechanganyika.
Mdogomdogo tutaleta mrejesho
 
Back
Top Bottom