Hayo ndiyo mafanikio yenyewe, ulipokuwa unaanzisha hiyo kazi ulikuwa na mategemeo na malengo,yanapotimia ndiyo mafanikio yenyewe. Mfano ulifungua genge ukaweka nia na juhudi ukijua baada ya miezi mitatu lau utakuwa unaingiza shilingi elfu kumi kwa siku, kweli baada ya miezi miwili unakuwa unapata faida ya shilingi elfu kumi na tano kwa siku...UMEFANIKIWA, unaendelea kuset malengo makubwa kiasi kwa hatua!
Tatizo ni kwamba watu wana dhana waliofanikiwa kibiashara ni matajiri/bilionea, sasa mimi mwenye genge nikiwambia nimefanikiwa wananiona kichaa, wakati mafanikio ni swala binafsi.