Wale wote waliokatishwa ndoto zao na TCU pitia hapa.

Wale wote waliokatishwa ndoto zao na TCU pitia hapa.

Nilikuwa kama wewe, nilikuwa napenda kuwa daktari tena ikiwezekana niendelee mpaka na masters hukoo... Nimekaa home miaka 2 nimeomba diploma CO vyuo vya serikali...kila nikiomba natemwa nikajisemea moyoni labda Mungu hakupanga niwe daktari labda Mungu ananiepusha na huko ninapotaka kwenda, nikabadilisha field nikatumia cheti cha form 4 nikaomba field za Engineering & Technology nimepata pale DIT first Round mapema tu...

Sometimes lazima ukubaliane kwamba Sio kila kitu kitime..sisi tunapanga, Mungu nae anapanga...nimefungua moyo wangu na sasaivi nafurahia huko ni apokwenda kuanza maisha mapya..
Ongera kapambane kiongozi
 
Kwanza kabisa udaktari ni wito kama walivyo masista na mapadre wale wakatolic nahisi mnanielewa vizuri. Kwahyo kuna wengine tuna maoenzi ya dhati kabisa katika jambo hili na sio kutafuta pesa tu.
Ni kweli kabisa... Cha msingi hakuna kukata tamaa kama kuna huo wito ndani yako.. kwahyo endelea kumwomba MUNGU tu hakuna kinachoshindikana kwake hta kama kwetu cc ikionekana ni vigumu.
 
Habari wadau na wakereketwa wote wa elimu ya bongo.

Mimi ni kijana mwenzenu ambaye TCU ishanikatisha ndoto za kuwa daktari si bongo tu dunia nzima MD ina ushindani sana. TCU guide book imetudanganya sana mwaka huu maelfu ya watanzania wamepoteza pesa zao katika application na baadh ya university zilikuwa na gharama kubwa mfano cuhas, kcmc ...... Can you imagine mtu anaomba MD vyuo karibia tisa 9 na hachaguliwi chuo chochote.

hila maisha ni popote usikate tamaa kwa kukatishwa ndoto zako. If the currently plan does not work change the plan but never change.
the goal .
Mungu atakusaidia utatimiza ndoto na malengo yako hila kama ni kwa mapenzi yake.
kuna wakati tunatakiwa kujitathimini kwa kina hapa naongelea hasa wale freshers na diploma's usiforce course ya kusoma kama hauna vigezo stahiki utapoteza pesa nyingi sana.

nawatakia mema wale wote waliopata nafasi ya kusoma University na college.
Hapa TCU mnawalaumu bure. Kusomea udaktari kwa Tanzania imekuwa shida sana na taizo si TCU bali upungufu wa nafasi. Kwa kushusha vigezo TCU wanawasaidia wale wanao taka kwenda kusoma nje hata wakirudi wanaonekana walikwenda wakiwa na vigezo vinginevyo ingekuwa shida kutambuliwa na TCU.
Dawa yake ni kunjenga shule zaidi za udakitari. Pia vijana wawe flexible wasing'ang'anie udakitari tu. TCU ingesaidia kutoa cutoff points za admission kwa kila course kwa mwaka uliopita kwenye kila chuo ili vijana wapime kina cha maji kable ya kutumbukia.
 
Back
Top Bottom