Wale wote wanaotumia bidhaa za kampuni ya Xiaomi tukutane hapa ili kupeana ujanja

Wakuu,
Kwanza kabisa shukrani Sana Sana kwa mchango wenu wa mawazo na ushauri Hadi mkanifanikishia kuagiza simu mpyaaa kabisa Aina ya Xiaomi Mi 7 global version.

Mzigo nimeununua Kwa Mi Store kwa pesa ya kitanzania,Tsh.322000 tu na hakika ni simu mpya kabisa Tena laini mno katika matumizi.

Niliagiza hii simu tarehe 04/10/19 na kwakweli huyu Mi Store alituma ndani ya siku mbili tu baada ya kuagiza.

Simu ikiwa pamoja na makolokolo kibaaao niliyoyaagiza kupilitia kwa sellers kibaaao wa AliExpress,nimefanikiwa kuipokea hapa posta ya wilaya yetu leo alasiri Tena bila malipo ya Aina yoyote(Kodi) huku siku 19 zikitumika katika mchakato wa kuipata,halafu huyu mtoa huduma wa posta, kaniambia niagize Tena [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Inawezekana kaikubali michakato yangu.All in all mashine ni tamu Sana kuitumia na ndo niliyotumia kuandikia maneno haya.
Asanteni Sana wadau.
Asante Sana mleta huu Uzi Mwenyezi Mungu akubariki Sana.
 
Hongera mzee ila hiyo ni Redmi 7 sio Mi 7, Natumai ngwe ijayo utaagiza Mi series ufurahie zaidi
Pia Hongera kwa uandishi mzuri [emoji3]
 
Mi niliagiza tarehe 7/10/2019, hadi tarehe 21 mzigo ukawa umeshatua bongo. Sasa sijui inachukua mda gani kufika posta ya wilayani kwetu.

 
Naomba Link ya Mi Store uliyenunulia mkuu.
 
Usijali ndugu kama sio super user hio redmi 7 inatosha mno mno kwa matumiz ya kawaida haijawahi kuniangusha kabisa mpaka sasa napeta nayo
 
Mkuu nahitaji betri ya s6edge plus..huku ghali sana..nimeambiwa ni 45K na sehem ingn ni 30K, moja inaitwa concorde na nyingn ni excellent!
Ipi ipo fresh kama unajua sehem
Kampuni za utengenezaji (OEM) battery ni nyingi na kusema ipi ni bora inakuwa ni kaz kidogo, kuhusu hiyo bei ni ya kawaida sana kwa battery zenye kiwango kizuri. Kama una hofu, kwamba unaweza kutoa pesa kubwa halafu ukapata betri yenye ubora hafifu ni bora ukatafute online.
 
Tokea wasitishe kuship L-ion sasa kupata battery Online mziki wake si wakitoto unless usibirie sellers shipping method za miezi 2
 
wakuu posta ya wilaya kwa upande wa Dodoma mjin nafanyaje kuijua au ndo mpk niguge
 
Inategemea unataka condition gani used au new, ila kwa ufupi bei zake zipo juu. Simu zao ambazo ni nafuu kidogo Pixel 3a ambayo kwa mpya ni $399 na used ni $315 bado shipping kuja TZ ambayo ni kama $50
Mkuu google pixels naweza pata kwa shiling I ngapi
 
Nimeingia aliexpress nimekuta kila empty
My order empty
Messeges empty
Cart
Shipped
Wish list
In dispute
Address
Zote hizo empty wakati niliagiza bidhaa ilikuwa ifike 25 - 30 october
Na kulikuwa na dispute seller mmoja hakunitumia mzigo
Naanza kukosa imani na hii mitandao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…