Wale wote wanaotumia bidhaa za kampuni ya Xiaomi tukutane hapa ili kupeana ujanja

Nini tofauti ya vioo vyenye Corning gorila glass na vya kawaida?
Cc Chief-Mkwawa
Gorilla Glass ina sifa ya kutopata mikwaruzo (scratch-resistant) na ni kioo kigumu sana vinatengenezwa na kampuni inaitwa Corning, aina hii ya vioo inatumika kulinda vioo vya simu, tablets na mobile devices nyingine. Kioo hiki ni chepesi kwa uzito lakini ni imara sana. Pamoja na uimara wote huo, vioo vya Gorilla Glass vinaweza kuwa vyembamba sana. Kama kifaa chako kina aina hii ya kioo haina haja ya kubandika kioo kingine kwaajili ya ulinzi wa skrini (tempered glass) kwa juu yake kwani chenyewe kinajitosheleza kulinda skrini yako kwa asilimia kubwa, hata kama wewe ni mtu wa kuweka simu yako pamoja sarafu au funguo, kioo hiki hakitaweza kupata mikwaruzo kwa uraisi. Tukija kwenye upande wa vioo vya kawaida visivyokuwa na protector fahamu kwamba kitakuwa na uraisi wa kupata mikwaruzo kwa haraka na kinaweza vunjika kwa wepesi, hivyo inakupasa kubandika tempered glass kwa ajili ya ulinzi wa skrini yako.
 
Mbona s6 edge zinavunjika sana zile nazo si zina hii sifa mkuu na je vipi nikiamua kuweka tempered glass.
 
Kuongezea hapa Gorilla glass zinaweza kuwa scratched na Quartz ambayo inapatikana rahisi kwenye vumbi

Madini yanapimwa ugumu kwa kutumia mohz na yanakuwa categorized kuanzia 1 mpaka 10. Dini gumu zaidi ni almasi na yenyewe ina maksi ya 10.

Kioo cha gorilla kinakuwa around 6 hakifiki 7 na quartz yenyewe ni 7 hivyo hii Quartz ina uwezo wa kuscratch vioo vya Gorilla.

Hivyo vumbi lililopo juu ya kioo cha simu yako likikutana na sarafu ama funguo simu yako itapata michibuko kirahisi.

Ndio maana hata kama mtu simu yake ina gorilla glass anaweka protector.
 
noted
 
Mbona s6 edge zinavunjika sana zile nazo si zina hii sifa mkuu na je vipi nikiamua kuweka tempered glass.
Simu ikipata mtikisiko mkubwa ni lazima ivunjike, gorilla glass hailindi kwa asilimia mia. Unaweza kuweka screen guard but kuna baadhi ya simu ukiweka protector inakuwa na sensitivity mbaya.
 
Simu ikipata mtikisiko mkubwa ni lazima ivunjike, gorilla glass hailindi kwa asilimia mia. Unaweza kuweka screen guard but kuna baadhi ya simu ukiweka protector inakuwa na sensitivity mbaya.

Mfano note 6 pro!...
 
Simu ikipata mtikisiko mkubwa ni lazima ivunjike, gorilla glass hailindi kwa asilimia mia. Unaweza kuweka screen guard but kuna baadhi ya simu ukiweka protector inakuwa na sensitivity mbaya.

Nillkin Tempered Glass
 
Chief sorry nipo nje ya mada ya xiaom tho me ni xiaomi useri[emoji120]
Naomba msaada wa jinsi ya kutoa security code ya nokia 3310?
 
Nikibadil line nikiwasha ndo inakuja,nkiweka line nayotumia siku zte hakzngui
Je hio line inayotaka security code ukiweka kwenye simu nyengine inadai pia security code?

Hapo kuna mambo mawili yanawezekana.
1. Ni line ndio ina hio lock hivyo inapodai code inakuwa ni ya line. Kutatua hili inabidi uwe na puk ya line kisha uwapigie mtandao husika. Kujua hili kama ni kweli fuata ushauri wa juu eka hio line kwenye simu nyengine kama kunatokea code kwenye simu nyengine pia tatizo ni line.

2. Hio simu ina lock ya mtandao wa simu, mfano simu za Tigo ama voda ambazo zimetengenezwa kutumia mtandao mmoja tu. Kujua hili eka line ya mtandao mmoja mfano unatumia kila siku tigo, jaribu kueka line nyengine ya tigo ikikubali eka line ya voda ama Airtel nayo uangalie kama itadai code basi simu imefungwa. Hapa itabidi utafute watu wanaotoa lock za simu uwatajie details watakazotaka kisha watakutumia unlock code,
 
Line nimetest kwny simu tofaut haina shida,nkaweka line nyingine ya mtandao huohuo stil ina password
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…