Gorilla Glass ina sifa ya kutopata mikwaruzo (scratch-resistant) na ni kioo kigumu sana vinatengenezwa na kampuni inaitwa Corning, aina hii ya vioo inatumika kulinda vioo vya simu, tablets na mobile devices nyingine. Kioo hiki ni chepesi kwa uzito lakini ni imara sana. Pamoja na uimara wote huo, vioo vya Gorilla Glass vinaweza kuwa vyembamba sana. Kama kifaa chako kina aina hii ya kioo haina haja ya kubandika kioo kingine kwaajili ya ulinzi wa skrini (tempered glass) kwa juu yake kwani chenyewe kinajitosheleza kulinda skrini yako kwa asilimia kubwa, hata kama wewe ni mtu wa kuweka simu yako pamoja sarafu au funguo, 8kioo hiki hakitaweza kupata mikwaruzo kwa uraisi. Tukija kwenye upande wa vioo vya kawaida visivyokuwa na protector fahamu kwamba kitakuwa na uraisi wa kupata mikwaruzo kwa haraka na kinaweza vunjika kwa wepesi, hivyo inakupasa kubandika tempered glass kwa ajili ya ulinzi wa skrini yako.