Wale wote wanaotumia bidhaa za kampuni ya Xiaomi tukutane hapa ili kupeana ujanja

Hii brand sijui nilichelewa wapi kuijua!!!

Kwa wale wasioweza kununua simu mpaka waone zimewekwa matangazo kwenye mabango kule Agrey na Uhuru basi watauziwa ma-refurbished mpaka akili ziwakae sawa.

Toka nimezijua simu janja sikuwahi kupata simu itakayonitoa stress za charge kila wakati,ila hii mashine natumia ninavyotaka,camera nzuri,muonekano smart yani ipo smooth data sizimi yaani nafanya vulugu ninavyotaka ile kuangalia angalia top bar kila wakati ili nijue charge imebaki percentage ngapi nimesahau.

Asante JamiiForums maana bila hii forum wala nisingejua hii kitu,tatizo mitaani watu wanakariri sana ukiomba ushauri wa simu ipi nzuri zaidi ya kuambiwa nunua Samsung,Huawei sijui Tekno au Infinix ambazo still zina matatizo mengi hakuna atakaekupa wazo linaloenda zaidi ya hapo,mpaka sasa nina vichwa viwili vimeachana na Samsung na iPhone wapo kwenye Xiaomi.

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
24 Dec Hadi 16 Jan ni siku 8?
Nijuavyo standard shipping AliExpress ikiwahi Sana Ni siku 12!!
Soma vizuri mkuu au kama ushawahi agiza mzigo nadhani unajua huwa unapitia stages zipi tangu kufanya malipo nimehesabu siku siku za hao singapore walivopokea na kuuleta TZ/Dar sijui umenielewa mkuu.
 
Soma vizuri mkuu au kama ushawahi agiza mzigo nadhani unajua huwa unapitia stages zipi tangu kufanya malipo nimehesabu siku siku za hao singapore walivopokea na kuuleta TZ/Dar sijui umenielewa mkuu.
Kwahiyo unataka kuniambia siku uliyonunua ndio seller katuma mzigo?
Nikubaliane nawe kwamba mzigo umefika Baada ya siku 8 nawe umeupokea ndani ya siku 23 inamaana posta waliukalia siku 14?
 
Kwahiyo unataka kuniambia siku uliyonunua ndio seller katuma mzigo?
Nikubaliane nawe kwamba mzigo umefika Baada ya siku 8 nawe umeupokea ndani ya siku 23 inamaana posta waliukalia siku 14?
Mkuu labda nisaidie hapa, order iliwekwa tarehe 24 desemba, ila seller hakuwa na mzigo, so tarehe 2 januari ndio aka process na kutuma mzigo,(mzigo ulikuwa shipped tarehe 2)
Ndani ya siku nane ndio mzigo ukafika Tz kuanzia siku mzigo ulipoanza kuwa processed.

Sijui umemuelewa mkuu.....
 
Muda wa kutuma mzigo ni siku 6 baada ya hapo order inakuwa cancelled labda buyer abonyeze kitufe cha kuongeza muda.
Swali linakuja je unaesabia siku ya kutumwa au tangu siku uliyolipa hela?
 
Muda wa kutuma mzigo ni siku 6 baada ya hapo order inakuwa cancelled labda buyer abonyeze kitufe cha kuongeza muda.
Swali linakuja je unaesabia siku ya kutumwa au tangu siku uliyolipa hela?
Inategemea na Mzigo Mkuu,kama simu nimeona waliweka 49 days (nahisi sababu ya sikukuu hizi).Me nimeagiza simu tangu tarehe 18 lakini mpaka leo seller hajatuma Mzigo nimewasiliana nae anasema atatuma Bado nasubiri. Na nimesoma kwenye reviews nimeona Kuna watu wanalalamika Mzigo ulifika ila seller alichelewa sana kutuma wengine zilikata hadi 2weeks.
Wangu sijui itafika siku ngp,maana nilivyoagiza sikuangalia tena process zinaendaje nikijua Mzigo upo njiani nakuja kucheki nikakuta bado hajatuma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Muda wa kutuma mzigo ni siku 6 baada ya hapo order inakuwa cancelled labda buyer abonyeze kitufe cha kuongeza muda.
Swali linakuja je unaesabia siku ya kutumwa au tangu siku uliyolipa hela?
Najaribu kufikiri mantinki ya huu mjadala ulio uanzisha hata siioni mkuu, sababu ufafanuzi umetolewa hapo juu. labda ungetuelewesha wewe umetatizika wapi kwa hoja ya mdau hapo juu. order kaweka 24 desemba (seller alikuwa out of stock) mzigo ukawa processed tarehe 2 january ndani ya siku 8 mzigo ukawa Tz hapo hajaweka siku ambazo posta walikaa na mzigo.
 
Mimi niliagiza simu tar 1 January 2019 seller akautuma tar 3 January, ulifika Tanzania tar 14 posta wakakaa nao mpaka tar 17 ndio nikaufuata mizigo kutokea Singapore nikiagiza inawahi
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kama seller ni FANTANCY TECHNOLOGY kuwa na subira atatuma...
 
Baadhi ya seller ni wazembe sana kutuma so ni jukumu lako kuwaimiza wafanye faster.
Mimi parcel zangu zinatumwa masaa machache baada ya kufanya malipo na wakichelewa hazipiti siku 4
 
Baadhi ya seller ni wazembe sana kutuma so ni jukumu lako kuwaimiza wafanye faster.
Mimi parcel zangu zinatumwa masaa machache baada ya kufanya malipo na wakichelewa hazipiti siku 4
Yeah Kuna wengine wapo faster kweli yani. Maana baada ya kuagiza simu siku mbili baadae nikaagiza Mzigo mwingine tena Cha ajabu huu mzigo wa pili ulitumwa siku ya pili yake wakati ule wa kwanza hata kua processed bado (mpaka leo)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kama seller ni FANTANCY TECHNOLOGY kuwa na subira atatuma...
Seller ni Zoe sijui,na store yake imeandikwa tu Mi Retail Store.

Halafu Sasa hivi nimetoka kucheki naona kwenye order mpya kaandika hatumi tena Mzigo kuja Tanzania,sasa sielewi kwa walioweka order awali inakuaje?!

Msauzy unanishaurije hapa, ni cancel order au nivumilie maana alinambia atatuma baada ya siku 10?!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Subiria hizo siku 10 zipite, kama bado hajatuma order itakuwa cancelled automatically. Kuwa mvumilivu tu, maana wao pia wanategemea mzigo kutoka kwa manufacturer, wanauza kwa njia ya Drop Shipping.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…