WALEZI: Tununue vifaa vya shule

WALEZI: Tununue vifaa vya shule

Raphael Thedomiri

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2019
Posts
442
Reaction score
729
Habarini wana-JF wenzangu.

Kama kichwa cha habari hapo juu kilivyo, ninawakumbusha wazazi/walezi wenzangu kwamba, tutenge muda mapema hii kuwanunulia watoto wetu vifaa vya shule, kuepuka gharama na usumbufu usio wa lazima.

===============

Zikiwa zimesalia wiki mbili muhula mpya wa masomo uanze Januari 9, bei ya vifaa muhimu imepanda huku wadau wa elimu wakisisitiza umuhimu wa wazazi kuvinunua kabla mahitaji ya vitu hivyo hayajapanda.

Vitu vilivyopanda bei katika Soko Kuu la Kariakoo jijini Dar es Salaam na maeneo mengine nchini ni mashati, suruali, kaptura, madaftari, masanduku ya nguo, mabegi na viatu.

Wakati vifaa hivyo vikipanda bei, ada katika baadhi ya shule binafsi zimeongezeka mpaka Sh500,000.

Kuhusu vifaa, wafanyabiashara hao wamesema, huenda vikapanda zaidi Januari kutokana na kuongezeka kwa mahitaji.


Mwananchi
 
Ungeturushia na mihamala ungekuwa umefanya la maana sana.

Watu wanapambana kupata pesa ya kula kwanza hayo ya shule ndio utayawaza leo?
 
Back
Top Bottom