Wali mayai wa kukaanga (Fried rice with egg pancake)

Goddess

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2014
Posts
7,397
Reaction score
25,806
Mahitaji: Mayai, wali, sukari.

Jinsi ya kuandaa:

Chemsha wali wako kama kawaida au hata kama unakiporo kitafaa,
Tia wali wako kwenye bakuli kubwa ambalo utachanganyia,
Kisha piga mayai wa 2_3 au upendavyo kutokana na kias cha wali unaotaka kukaanga.
Kisa tia sukari 2Table spoon.

Changanya na mchanganyiko wako uko tayari kwa kupikwa.

Ziada: unaweza kula kwa breakfast au upendavyo

20191009_123617.jpg
 
Unamaanisha ni kama unapika chips zege?

je naweza kuweka chumvi badala ya sukari?

Ni asili ya wapi hiki chakula?
 
Kuna siku nina kiporo changu cha ubwabwa na rost la maini ila nikajisikia kama kula cha tofauti hivi. Wazo likanijia kupika hivi ulivyopika ila niliweka chumvi na kikawa kitamu tu na ka juice ka embe.
Kumbe ni chakula kabisa kinapikwaga[emoji134][emoji134][emoji134]
 
Nilishawahi kupika kwa kutumia hii recipe yako Goddess nilitaka kuweka mrejesho huu uzi ukaoneshwa umefungwa na wewe ulipigwa ban ni muda kidogo ilikuwa.
Mimi niliweka na mayonnaise tomato na pepsi baridi ilikuwa tamu mno

mama wawili
 
Aiseee hongera kwa kujaribu pishi[emoji3531] ile ban sitaki kuikumbuka[emoji38]
 
  • Thanks
Reactions: amu
Sawa ngoja sie tunaojuwa kupika chai ya rangi na mayai ya kukaanga tu tuwe wapenzi wasomaji.
 
Aiseee hongera kwa kujaribu pishi[emoji3531] ile ban sitaki kuikumbuka[emoji38]
Sasa ndo hadi uzi wako wakauzuia?
Nilishangaa sana jamani.
Nilipika.kilibaki kiporo cha wali.
Nikapika zangu tukashushia na pepsi big [emoji39][emoji39] tamu sana.
 
Mahitaji: Mayai, wali, sukari.

Jinsi ya kuandaa:

Chemsha wali wako kama kawaida au hata kama unakiporo kitafaa,
Tia wali wako kwenye bakuli kubwa ambalo utachanganyia,
Kisha piga mayai wa 2_3 au upendavyo kutokana na kias cha wali unaotaka kukaanga.
Kisa tia sukari 2Table spoon.

Changanya na mchanganyiko wako uko tayari kwa kupikwa.

Ziada: unaweza kula kwa breakfast au upendavyo

View attachment 1229811
naukaang kwa mafuta au bila mafuta?
 
Nilishawahi kupika kwa kutumia hii recipe yako Goddess nilitaka kuweka mrejesho huu uzi ukaoneshwa umefungwa na wewe ulipigwa ban ni muda kidogo ilikuwa.
Mimi niliweka na mayonnaise tomato na pepsi baridi ilikuwa tamu mno

mama wawili

Uliweka chumvi ama sukari.
Ama uliweka vyote kama tunavofanya kwenye chapati za maji
 
Back
Top Bottom