Ndagullachrles
Senior Member
- Jun 20, 2023
- 153
- 161
"Tunaomba mtusaidie kunusuru maisha ya watoto wetu hii shule ni kama imegeuzwa Kambi ya mateso kwa watoto wetu".
Hii ni kauli ya mmoja wa wazazi wenye watoto katika shule ya sekondari Wali iliyopo wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro.
Shule hiyo inamilikiwa na Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha mapinduzi (CCM) ambayo licha ya kufanya vizuri kwenye elimu na kuwa na ufaulu mzuri,inalalamikiwa na wazazi kuwa imekuwa ikitoa adhabu Kali kwa wanafunzi na baadhi ya wazazi wamelazimika kuwaondoa watoto wao kwenye shule hiyo .
Shutuma nyingi zimeelekezwa kwa uongozi wa shule hiyo iliyopo chini ya mkuu wake wa shule Steven Luhende kwamba imekuwa ikitoa adhabu kali kwa wanafunzi ambazo zinakiuka hata miongozo na walaka wa elimu unaotoa maelekezo ya namna ya kutoa adhabu kwa wanafunzi .
Baadhi ya wazazi wanataka ofisi ya Ofisa elimu wa wilaya ya Hai ,Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Hia kuiangazia shule hiyo kwani ikiachwa ikaendelea na mfumo wake wa utoaji adhabu Kali ipo siku yatatokea ya kutokea .
Wakati hali ikiwa hivyo,Katika tukio la hivi karibuni kijana mmoja ambaye amemaliza kidato cha Sita shuleni hapo hivi karibuni alijikuta akinyimwa cheti chake baada ya kuingia eneo la shule hiyo akidaiwa kuwa na nywele ndefu .
Kijana hiyo alisotq kwa zaidi ya masaa Saba na licha ya jitihada za ndugu zake kutaka apewe cheti ili awahi chuoni jitihada hizo hazikuzaa matunda.
Hatua hiyo ililazimu uongozi wa juu wa Chama cha Mapinduzi(ccm)mkoa wa Kilimanjaro kuingilia kati na kuagiza kijana huyo apewe cheti chake.
Hata hivyo kibao kikageuka tena kwa Kijana huyo kuzushiwa jambo kwamba wakati anamaliza shule alikuwa anadaiwa pesa sh,50,0000 ambazo uongozi wa shule hiyo unadai zinatokana na uharibifu wa vitabu vitano.
Kutokana na umhimu wa cheti hicho kijana huyo alilazimika kufanya mawasiliano na ndugu zake ili waweze kumlipia pesa hizo na baada ya malipo kufanyiwa hatimaye akapewa cheti chake lakini hakupewa stakabadhi ya malipo na kuhoji kwa nini asipewe.
"Hebu muulize Mkuu wa shule kama alikuwa anadaiwa waliwezaje kumpa Results Slip na Leaving Certificate,Leo wanakuja na hadithi za kudaiwa elfu hamsini ,huu ni wizi na kwa nini wamemnyima risiti ambayo ni Hali yake kupewa?,anahoji mmoja wa watu wa karibu na kijana huyo.
Kazi kwenu mamlaka za elimu ,wazazi wanalalamika mateso ya watoto wao ,Sasa chukueni hatua.