Uchaguzi 2020 Walikuwa hawaamini kama upepo umebadilika

Joined
Feb 18, 2019
Posts
53
Reaction score
539
Walikuwa hawaamini until Lissu kaenda Dodoma ndio vichwa vimewakaa sawa. Kila kona anakopita nyomi kama lote, tena lile la hiari hamna anayebebwa wala kulazimishwa kwenda kwenye mikutano.

Nimesikia kwenye baadhi ya maeneo mnawalazimisha watumishi kwenda kwenye mikutano yenu. Naomba niwaambie tu hiyo ni kama kujitekenya na kuchema mwenyewe.

Huwezi kukwepa ngumi ya uso kwa kufumba macho. Fungueni macho muone uhalisia wa mambo. Upepo umebadilika na hakuna njia yoyote inayoweza kubadili uelekeo wa upepo.
 
Mambo ya aibu sana. Jiwe alifikiri akiwashawishi kwa vyeo na fedha Wabunge na Madiwani toka Upinzani basi watakuwa wamewapata na Wafuasi wao.

Madaraka na rasilimali za nchi alizitumia kupanda mbegu ya chuki na ubaguzi sasa acha avune alichopanda.
 
Wanatia huruma, watumishi wa umma tunalazimishwa kuhudhuria mikatano yao, halafu tunaonywa tusihudhurie mikutano ya upinzani. Ila tumeshaamua, tutahudhuria tu mikutano yao lakini tar 28 October tunajua cha kufanya.

Halafu Wana Hali mbaya, taasisi za serikali na binafsi pamaoja na matajiri wanalazimishwa kuchangia kampeni zao tena kwa kupangiwa kiwango. Huu ni uhuni, mwisho wenu unakuja.
 
Aise nyie watu mna vituko Sana, yaani hao watu wa Mbeya ndio mnaona watafanya Magufuli ashindwe. Hao watu aliopata Mwanza subiri uone Majibu yenu leo, hao watu aliopata Mbeya Magufuli anapata zaidi. DSM wameshamkata, Dodoma juzi alihutubia miti, mtaugua pressure bure!
 
Ila mwaka huu tumebanwa sana tofauti na mwaka 2015. Na hivi Magu amekataa uvccm kumpigia kampeni, akina nape, kibajaji ,makamba walio zoea kuzunguka nchi kila mwaka wa kampeni wamepigwa stop, mzee baba anazunguka na sekretariat tu. Akina Nape walijua wataitwa mzee baba kakomaa anachanja mbuga tu, hataki zile habari zenu sijui tulikupigania mzee
 
CCM walidhani Lissu ni mwepesi kumbe ndiyo wamejiingiza kwenye maji yenye kina kirefu chenye mamba wakali.

Jana Mama Maria Nyerere ndiyo kabisa amewavua CCM nguo ya ndani bila aibu tena hadharani 🤣🤣🤣
Kasemaje mama maria
 
Aise nyie watu mna vituko Sana, yaani hao watu wa Mbeya ndio mnaona watafanya Magufuli ashindwe. Hao watu aliopata Mwanza subiri uone Majibu yenu leo, hao watu aliopata Mbeya Magufuli anapata zaidi. DSM wameshamkata, Dodoma juzi alihutubia miti, mtaugua pressure bure!

Hebu pumzisheni wasanii hata kwa siku moja tu halafu tuone kama mtavutia watu nyie zaidi ya wazee na kinamama masikini.

Hebu mthubutu mle aibu. Kila sehemu kumekaa vizuri. Kura zikipigwa kihalali mnalizwa. Hata mkijaribu ule upuuzi wenu wa siku zote tayari mmechelewa maana mbinu zote zimeshanaswa.
 
Walikuwa hawaamini until Lissu kaenda Dodoma ndio vichwa vimewakaa sawa. Kila kona anakopita nyomi kama lote, tena lile la hiari hamna anayebebwa wala kulazimishwa kwenda kwenye mikutano.

Nimesikia kwenye baadhi ya maeneo mnawalazimisha watumishi kwenda kwenye mikutano yenu. Naomba niwaambie tu hiyo ni kama kujitekenya na kuchema mwenyewe.

Huwezi kukwepa ngumi ya uso kwa kufumba macho. Fungueni macho muone uhalisia wa mambo. Upepo umebadilika na hakuna njia yoyote inayoweza kubadili uelekeo wa upepo.
Upepo umegeuka mitandaoni au kwenye kampeni live.
 
Taharuki kubwa imeingia ndani ya CCM.
Maji yameanza kuzidi unga, ugali waupikwi tena.

Leo asubuhi naona Kassim Majaliwa katinga kanisani (kituo cha redio safina, Arusha) kuomba radhi baada ya jana serikali kuzuia Kongamano la maombi lililoandaliwa na kituo cha redio Safina (Mbauda, Arusha) ili raia wasombwe kwenda kwenye mkutano wa CCM. Hasira zikawajaa waumini wa kikristo kupita kiasi.
 
Walikuwa hawaamini until Lissu kaenda Dodoma ndio vichwa vimewakaa sawa. Kila kona anakopita nyomi kama lote, tena lile la hiari hamna anayebebwa wala kulazimishwa kwenda kwenye mikutano.

Nimesikia kwenye baadhi ya maeneo mnawalazimisha watumishi kwenda kwenye mikutano yenu. Naomba niwaambie tu hiyo ni kama kujitekenya na kuchema mwenyewe.

Huwezi kukwepa ngumi ya uso kwa kufumba macho. Fungueni macho muone uhalisia wa mambo. Upepo umebadilika na hakuna njia yoyote inayoweza kubadili uelekeo wa upepo.

Mnaminya uhuru wa habari tumewaacha.

Safari hii wizi wa kura hatukubali. Safari hii mshindi katika sanduku la kura mtamtangaza.
 
Back
Top Bottom