Walimu acheni tamaa za ovyo

Walimu acheni tamaa za ovyo

TheForgotten Genious

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2014
Posts
2,087
Reaction score
3,156
Siku hizi shule nyingi za Serikali msingi na sekondari hasa za kutwa walimu wanawafanyisha wanafunzi mitihani kila baada ya siku 3 na wanalipa 1200 au zaidi.

Hivi kila baada ya siku tatu kipi kipya wanakuwa wamefundisha watoto mpaka wawafanyishe mitihani? Hivi kufanya mitihani kila mara ni kipimo cha uelewa?

Ni kweli maslahi yenu ni madogo lakini msichukulie sababu ya kufanya uhuni, hata kama maslahi madogo hakuna mtu aliwachagulia hiyo kazi.
 
Wazazi wenye akili mgando, mwanao anafanya mitihani anapata sharpness na kuzoea mitihani mzazi analalamika.

Tutafte pesa kwa bidii wanajamii forum wenzangu, sasa sijui hio 1300 kwa mwezi hata elfu 10 haifiki ndo kitu Cha kulalalama tena kwenye elimu ya mwanao? Kila mtu anajua anakula vipi kazini kwake, sioni tatizo walimu wakipata chochote kitu ilhali wanasaidia wanafunzi.

Msione Kila siku kemebos sijus st Francis wanaleta division 1 cream mnalalamika sijui wanaiba mitihani, Hawa watoto wanafundishwa haswa na wanaofanya mitihani Kila wiki, hata kama wanafanya ujanja bado ni kuwaboost wanafunzi ambao wapo sharp, mitoto kama ya taifa sekondari hata ukiyapa mitihani inayofanya kesho ilale nayo bado Kuna mingine itafeli tu, maana unakuta hata English changamoto.

Wazazi tuachane kulalama Dunia imebadilika , mnalia Lia hizo elf 10 kwa mwezi wakati nursery watu wanalipa zaidi ya milion 2 kwa mwaka, shauri yenu na watoto wenu bana.

Nimesahau kitu, PUMBAVU!
 
Sasa walimu unakaa nao mtaani kwako,unakuja kutuambia sisi huku...

Hivi unadhani walimu watatajirika na hicho kibuku chako unachotoa?

Mkuu walimu wanamaisha magumu sana hyo buku haiwafikishi popote...
Hayatuhusu si maisha yao, sasa wanataka watupelekeshe sisi? Si walichagua wao wenyewe kuwa walimu?
 
Wazazi wenye akili mgando, mwanao anafanya mitihani anapata sharpness na kuzoea mitihani mzazi analalamika,



Nimesahau kitu, PUMBAVU!!
Usitudanganye we paka aliyekwambia mitihani inaleta sharpness nani? Kwa asilimia zote,,tamaa na shida za hovyo zinawasumhua,kuna muongozo wa elimu unaeleza ni kiasi gani cha mitihani mwanafunzi anatakiwa apewe na kila baada ya muda flani,usitujaze upepo
 
Butimba sekondari ya mwanza michango ni kama ifuatavyo.
1. Gharama za photocopy- 5000@month
2. Gharama za chakula-30000@month
3. Gharama za tuisheni-1000@month
4. Gharama za walimu wa kujitolea- 2000@month
5. Tisheti - 12000
6. Rim papers-16000 as per now.
Jumla kuu: kwa mwezi ni 38,000/ ukitoa tisheti na rim zinazojumuishwa kwenye grand total ya mwaka mzima.
Hapo mzazi hajagharamikia nauli ya mwanae.
Kweli walimu wameamua kunyoosha makucha.

Mwisho kabisa. Wanafunzi wa form one hawasomi na mkuu wa shule amedai watafundishwa masomo mawili tu mwaka huu,
Hesabu Na kiingereza.

Rais Samia toa ajira usaidie watoto wa watanzania.
 
Sijakuelewa mkuu
Hivi ni hupendi mwanao afanye mtihani kila baada ya siku 3 au huna iyo shs 1200 ya kulipa kila baada ya siku 3?
Mimi kwanza wanangu hawajawahi kusoma huko ,na hiyo 1300 si kitu kwangu,nazungumzia lengo la wao kutoa mitihani si watoto wafanye mitihani bali mchongo wakupata pesa,imagine hata kufanya masahihisho ya mtihani wanataka pesa tena
 
Butimba sekondari ya mwanza michango ni kama ifuatavyo.
1. Gharama za photocopy- 5000@month
2. Gharama za chakula-30000@month
3. Gharama za tuisheni-1000@month
4. Gharama za walimu wa kujitolea- 2000@month
5. Tisheti - 12000
6. Rim papers-16000 as per now.
Jumla kuu: kwa mwezi ni 38,000/ ukitoa tisheti na rim zinazojumuishwa kwenye grand total ya mwaka mzima.
Hapo mzazi hajagharamikia nauli ya mwanae.
Kweli walimu wameamua kunyoosha makucha.
😅😅😅
 
Back
Top Bottom