Walimu acheni tamaa za ovyo

Sawa,haturudii tena
walimu zidisheni mitiani ya kutosha ,
hili la shule kutokuwa na mashine za kuchapa mitiani haya ndio mambo ya kuzungumza si kina lema wanatukana bodada na kujisifia kuvaa chupi na kadeti za kisasa
 
Watumie pesa wanazopewa na Serikali na sio kutoza wanafunzi
Unajua ratiba ya mitihani kwa mujibu wa fedha zinazokua allocated na serikali Ni mingapi?
Ni mitihani minne tu!

Kwahiyo kwa maana ya fitness test mwalimu atumie mshahara wake kununua rim, kuchapa mtihani, kudurufu mitihani na kusimamia kwa muda wake amark na arudishe matokeo plus correction?

Nenda kwenye Shule za kulipia Kuna weekly au Monday tests, Kuna Continues Assessment Tests (CAT) Inayofanyila monthly, Kuna Pre-midterm test halafu Kuna hiyo midterm test halafu Kuna self assessment za mwalimu wa SoMo peke yake!

Mpaka huyu mwanafunzi aje kufanya mitihani kwa mujibu wa ratiba ya serikali anakua tayari ameinternalize kila kitu katika topic au mada husika kwahiyo pass Mark y lazima iwe above 75%
Ufanyaji wa mitihani hiyo Ni kwamba shule inahakikisha imeprovide all necessary facilities kwa ajili ya mwalimu kuhakikisha malengo yake yanatimia, ya shule yanatimia pamoja na ya mzazi na mwanafunzi

Ndugu hizo Shule zinaitwa community schools yaani shule za umma kwahiyo ili upate ufaulu mzuri lazima hiyo community iwe responsible kwa kila kitu, serikali inajenga madarasa, kuweka madawati na kuleta walimu na chaki! Mengine mtajua wenyewe ikiwemo chakula na Mambo mengine.
Kama hujui Kama nchi hii Ina shule ya Aina nne endelea kupiga kelele:

1. State schools (Tambaza, Tabora Boys Ashira, weru weru Bunge, Olympio nk. Huko hutasikia wakimtuma mtoto rim au buku ya msosi! Kila kitu Ni budget ya serikali

2. Community Schools, Ni hizo unazolalamika bila kujua kwamba ninyi ndo mnahusika!

3. Kuna institutional schools shule za taaissi za dini na nyinginezo ikiwemo shule za CCM

4. Shule za watu binafsi!

Category number 2-4 huko inatolewa elimu na Kuna uwekezaji mkubwa wa fedha na rasilimali watu!

Number 1 ndiko uliko wewe, wakati unakenua meno elimu Bure tambua kwamba Elimu Ni Ghali na Elimu Ni gharama Kama ilivyo Afya!
Huko kwenu wanahudhuria shule na sio kwenda kujifunza.

Kwahiyo Kama unaona elimu Ni Ghali jaribu ujinga!

Elimu bure Ni bure kwasababu hakuna maarifa yoyote wanayopata wahudhuriaji!
 
nimesikitika sana mtu analalamika mtiani kila bada ya siku tatu ni mingi!
kwa jinsi masomo yalivyo na mada nyingi tena ndefu hilo alifikirii ,elimu bora ni pamoja na kumpima mwanafunzi kwa kila ulicho fundisha ,na njia nziri ni kumpa mtiani .tukisema kusiwe na mitiani mingi ya ndani tusubiri ya muula na kitaifa sijui ni elimu gani iyo.
 
Pole sana ndugu, hakuna namna waalimu nao wanahitaji posho za kujikimu kwa hio lazima wawakamue wazazi kidogo
Kuna shule kimara walimu walikuwa wanatoza sh500 ya mtihani mmoja kila siku na 1500 kila jumamosi
hapo unakuta mzazi ana watoto watatu shulenu na biashara yake haimpi faida ata ya 10,000 kwa siku

mzazi mmoja kimya kimya akaenda kushtaki wakaguz wa elimu wakasimamisha kufanyika kwa hio mitihani
 
Kwanini wasifanye bure hizo tests..

Hapa tunapinga kuwekwa kiwango cha pesa sh 1200 kila tests.
Hatupingi kufanya tests.

Kama ingekuwa tests bila pesa hata kila siku wafanye tu.

RIP MAGUFULI,,,huu upuuzi ulikoma kabisa mashuleni.

Sent from my 2201117SG using JamiiForums mobile app
 
Wanachokifanya wanaitisha kikao cha wazazi kisha wanawapa maelezo meengi mpaka wazazi wanachanganyikiwa mwisho wanawaambia wazazi wawe wanachangia. Wazazi kwa kuhofia watoto wao kufeli wanakubali matokea kila siku tunachangishwa. Sasa kwa Dar kila mtihani wazazi wanalipia kwa hiyo ile pesa za elimu bure sijui zinakwenda wapi. Mpaka mock ya wilaya na mkoa tunachangishwa wazazi.
 
Hizo shule za serikali na hasa zile za Kata, zina changamoto nyingi za kifedha kuliko hata unavyofikiri. Nina rafiki yangu wa karibu ni mkuu wa shule, analalamika mpaka basi.

Na wakati huo huo unatakiww ufaulishe wanafunzi wote. Sasa usipotumia njia za aina hii, hao wanafunzi watafaulu vipi?
 
Tafuta pesa kijana, huwezi kuja kulia Lia kwa wanaume kisa sijui 1300 kwa wiki, na we unaitwa baba? Afu mtoto wako anasoma shule ambayo huna contants za walimu wake? Kama imekuuma sana piga simu shuleni, narudia tena PUMBAVU!!
...Mkuu, ukiwa na Vipesa Haina maana ukubali kuvitoa toa Kwa sababu ubavyo !.
 
Kwamba hawalipwi mishahara au wana changamoto gani?

Siku hizi wamezusha mtindo mwingine kulazimisha wanafunzi Kula lunch zinazopikwa hapo shule mchana na wanataka 20,000 kila mwezi..
Kwa kila mwanafunzi,,,

Huoni kama wanazidisha mzigo kwa wanainchi?
Hivi utalazimishaje mtoto ale shule Saa 7 mchama wakati nyumbani akirudi Saa 9 atakuta chakula?

Why walimu why?

Sent from my 2201117SG using JamiiForums mobile app
 
Kula kwa urefu wa kamba
 
Mwalimu acha njaa
 
Mwalimu acha njaa
Sio teacher ila nyi ndo muache njaa, hizo sio pesa za mwanaume mtafutaji kuja kulia mbele za wanaume

Hio pesa ya mwezi Wavivu camp hata bia Moja hunywi hapo, tafuteni hela pumbavu
 
Sio teacher ila nyi ndo muache njaa, hizo sio pesa za mwanaume mtafutaji kuja kulia mbele za wanaume

Hio pesa ya mwezi Wavivu camp hata bia Moja hunywi hapo, tafuteni hela pumbavu
Kwamba hata kama una mamilion yai pesa, ziliwe na watu bure bure tu.

Kama unataka pesa za bure Si tufanye makubaliano tu.

Kwani VASELINE sh ngpi?.
.
Yaani kabisa unashauri pesa za wanaume wenzio zitoke burebure bila jasho upewe.

Sent from my 2201117SG using JamiiForums mobile app
 
Kula kwa urefu wa kamba
Hatari Sana,,

Halafu mbaya zaidi Ktk kila shule ya serikali Kuna kigenge cha wahuni wapigaji wamejivika mwamvuli wa uongozi wa umoja wa wazazi wa wanafunzi.


Hawa ndy chawa na walamba asali mashuleni,, wanakula pamoja na walimu ,,

Wanapanga maamuzi kama vile wazazi wote wameafiki maamuzi hayo..
Ukiwabana kwa hoja mkutanoni watakushambulia kama nyuki mradi watimize Azma yao ya upigaji.

Sent from my 2201117SG using JamiiForums mobile app
 
Wanakwambia walimu wanatosha
 
1300 kwa wiki kwa mtoto kufanya mitihani ndo unalalama? Sasa unaishi maisha Gani? Kua makini kwa umaskini huo utakuja kupakatwa pumbavu
 
Umenikimbusha mwalimu wa hesabu primary alitupa maswali kama zoezi la kawaida na akafanya correction halafu akatuanbia huu ndio mtihani wa kesho nimeuleta kama nilivyoutunga. Natumai kila mtu atapata [emoji817]. Lengo sio kuvujisha mtihani kwani aliandika hadi maelezo ofisi ya mtaaluma. Akatwambia atakayepata chini ya 70 kazi anayo.

Kesho yake mitihani ya muhula wa kwanza inaanza tunaletewa mtihani wa hesabu ukiwa vilevile alivyoahidi mwalimu kuanzia swali la 1 hadi la 50. Nifupishe story, robo tatu ya darasa walifeli nikiwemo mimi niliyepata aibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…