Walimu Arusha watakiwa kwenda uwanjani Sheikh Amri Abeid kesho kwaajili Rais Samia

ESCORT 1

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2015
Posts
1,412
Reaction score
3,043
Kesho kunafanyika maadhimisho ya wiki ya Usalama barabarani mkoani Arusha ambapo mgeni rasmi ni Rais Samia Suluhu Hassan.

Katika kuhakikisha shughuli hiyo inafana, walimu wote wa shule za sekondari na msingi Arusha, wameagizwa kwenda kuhudhuria bila kukosa shughuli hiyo.

Walimu pekee ambao hawatatakiwa kwenda ni wale wanaosimamia mitihani ya kidato cha nne inayoendelea.

My take:
Naona ni impact ya wananchi wa chini wakiwemo machinga kutokumsapoti mama, hivyo wakaona uwanja unaweza ukawa mtupu
 
Kulikuwa na machaliiiii wa Magufuli,Hao hawataweza kuhudhuria kwaniaba ya walimu?
 
Sherehe za Usalama barabarani, Walimu wanakwenda kufundishwa dhana ya Usalama wetu Kwanza au?
 
Sijui kwenye kampeni zake 2025 itakuwaje? Itabidi kukodi watu nje ya nchi.
 
Yale yale ya mwendazake. Sasa ukanilazimishe nije kukaa juani!? Nipigwe na jua kweli

Kwa hiyo kifupi kesho shule hakuna, na wanafunzi watamisi vipindi kisa MAMA yao.
 
Huyo mama ni nyota ya mavii abebeki huwa nacheka sana kusikia wapumbavu wa chama chake wakitaka kumnadi kama mgombea uraisi 2025
 
Kwahiyo hautaki Waalimu wakaonane na Mwajiri wao? Sasa shida zao watampa nani kama wakimkwepa Mwajiri?

Wangesema toka mwanzo wa school year wakati walimu wanaandika kalenda ya kusomesha.

Huku ni kutojali elimu ya watoto kwenye public schools. Viongozi wetu wa nchi za Kiswahili masikini ya Mungu, hawajui wajibu wao kabisa.
 
Mama na kaskazini...kaskazini na Mama..
 
Juz kaja mwanza bugando, muda mfup tu katimua. hakulala ata siku moja. Jion tukasikia yuko Zanzibar. Kwann alifanya hvyo?, Kwsbb anajua kinacho endelea ndan ya mioyo ya watu....
 
Mama na kaskazini...kaskazini na Mama..
Aweteue basi kwenye uongozi wake....bila kuwatea akaendelea kuteua kutoka visiwani (Zanzibar) na kanda ya Pwani hayo ni maigizo
 
Huu upuuzi kumbe bado unaendelea?

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Walimu wanafanywa kama masanamu vile.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…