Dazzle
JF-Expert Member
- Dec 26, 2013
- 214
- 56
Kama umezoea wizi basi utaendelea kuiba tu.Wiki mbili zilizopita wanafunzi wa chuo kikuu Iringa walianza kufanya UE au University Examinations.
Cha ajabu wale tunaotegemea wakawafundishe wadogo zetu yaani waalimu baadhi yao ndio wameiba mitihani ya UE. Hawa sio wengine bali ni baadhi ya wanafunzi wa Ualimu mwaka wa 3.
Swali langu kwetu mliofanya huu ujinga tutegemee nini mtskapofika huko kuwafunza wadogo zetu? Je mlikuja kusoma au kuiba mitihani?
Rai yangu kwa uongozi wa chuo, chukueni hatua kali kwa wahuni hawa wa elimu. Kila aliyehusika kuanzia wafanyakazi au lecturers kama wapo na wanafunzi husika wapewe adhabu kali ili kulinda heshima ya chuo.
Pia wezi hawa wakumbuke kuwa hawakuja Iringa kwenye starehe wamekuja kusoma na kama ndio hivyo kitendo cha kuiba mitihani ni uhuni usiovumilika. Kama mmezoea kuiba basi fani ya ualimu haikufai rudi kwenu ukawe mpiga debe au teja.