Walimu Iringa University waiba mitihani

Walimu Iringa University waiba mitihani

Dazzle

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2013
Posts
214
Reaction score
56
Kama umezoea wizi basi utaendelea kuiba tu.Wiki mbili zilizopita wanafunzi wa chuo kikuu Iringa walianza kufanya UE au University Examinations.

Cha ajabu wale tunaotegemea wakawafundishe wadogo zetu yaani waalimu baadhi yao ndio wameiba mitihani ya UE. Hawa sio wengine bali ni baadhi ya wanafunzi wa Ualimu mwaka wa 3.

Swali langu kwetu mliofanya huu ujinga tutegemee nini mtskapofika huko kuwafunza wadogo zetu? Je mlikuja kusoma au kuiba mitihani?

Rai yangu kwa uongozi wa chuo, chukueni hatua kali kwa wahuni hawa wa elimu. Kila aliyehusika kuanzia wafanyakazi au lecturers kama wapo na wanafunzi husika wapewe adhabu kali ili kulinda heshima ya chuo.

Pia wezi hawa wakumbuke kuwa hawakuja Iringa kwenye starehe wamekuja kusoma na kama ndio hivyo kitendo cha kuiba mitihani ni uhuni usiovumilika. Kama mmezoea kuiba basi fani ya ualimu haikufai rudi kwenu ukawe mpiga debe au teja.
 
Tatizo la kuiba mitihani naona limekuwa sugu kwa wanachuo, na ili linaletwa na wale wanaofika chuo kwa kuunga unga vyeti siku sinyingi nimeona uzi wa chuo cha SEKOMU na wao wameiba mtihani tena mwaka wa tatu kitivo cha elimu.

Pia na malecturers wanaojiusisha na swala la mapenzi na mabinti wanaweza kuwa source.
 
Sodium,

Pumbavu Wewe Nyamaza Hujui Ki2, Mimi Nimefika Chuo Kwa Kuunga Unga Mbona Sijaiba Mtihani? Pili,ingekuwa Wanaofika Chuo Kwa Vyeti Vya Kuunga Unga Iweje Wafike Chuo Kwa Kuunga Unga Ili Hali Wanaiba Mitihani Kwanini Wasifaulu?
 
Last edited by a moderator:
Pumbavu Wewe Nyamaza Hujui Ki2, Mimi Nimefika Chuo Kwa Kuunga Unga Mbona Sijaiba Mtihani? Pili,ingekuwa Wanaofika Chuo Kwa Vyeti Vya Kuunga Unga Iweje Wafike Chuo Kwa Kuunga Unga Ili Hali Wanaiba Mitihani Kwanini Wasifaulu?

Hapa nakubaliana na wewe wako wengi wakati wanamaliza form 4 hawakufanya vizuri wakarudia mtihani wakapita na form six wengine ikawa hivyo hivyo lkn leo wako chuo na wanafaulu vizuri bila kuiba mitihani.

Wizi ni tabia ukiwa nayo utaiba tu na mwizi akikosa cha kuiba anaweza hata kujiibia mwenyewe.mwaka wa tatu unaiba mtihani?shame on u
 
Walisimamishwa masomo kwa kipnd kirefu soo exception yao kubwa ikawa hawataweza kufanya paper koz ya kukosa mda wa kusoma..? Nadhani kwanza mimi kama mwanafunz chuo wa UoI wangewapelekea mbele UE ili wapate muda wa kujiandaa na sio kupewa paper...?
 
Wapi Rev. Rich Lubawa ausemee wizi huo uliofanyika ofisini kwake kwani yeye ndio mtaaluma mkuu wa chuo ati! Nilipita hapo kwa shahada ya kwanza na sikuwahi kusikia au kuyaona hayo kwani walikuwa very strict.

Wahusika wawajibishwe kwa uzito wa makosa yao ili kuiweka sawa heshima ya chuo changu.
 
Inamaana walimu wameiba mitihani yote? Na je, iliwezekana vipi? Wahusika hawajulikani? Na kama wanajulikana ni akina nani na wanamahusiano yapi na waliandaa mitihani?
 
Hao ni wazembe tu mbona wakat tunasoma tulikaa nyumbani mwaka mzima then tuliporudishwa chuo tumefika kama Leo kesho take tukafanya UE na tukafaulu vizuri?halo wachukuliwe hatua za kinidham ili kukomesha tabia hiyo.
 
Tumaini Iringa haina utamaduni wa kumfukuza yeyote kwa kosa lolote

Utamaduni huwa nao unabadieika kidogo siku zinapoenda hasa mabadiliko mengine ya taasisi yoyote. katika hili naona mwaka huu hakuna msalie mtume. watu wataondoka .
 
utamaduni huwa nao unabadieika kidogo siku zinapoenda hasa mabadiliko mengine ya taasisi yoyote. katika hili naona mwaka huu hakuna msalie mtume. watu wataondoka .
Lubawa, Nikolasi Bangu, Mdegela na wahuni wengine wenye mamlaka hawana ubavu wa kufukuza mtu
 
Lubawa hayupo yupo dvcaa mwngn....uongoz mbovu!!iv hamjiuliz walimu wameibaje mitihani?uko juu wnyw wana mabifu yao wameamua kuchafuana kwa kugawa mitihan kwa wanafunz
 
Hawa wezi wamewagharimu wenzao kesho wanarudia mtihani.

Nyambafu ningekuwa mimi msahihishaji mngenikomaa hasa wezi wa elimu.
 
Back
Top Bottom