A
Anonymous
Guest
Sisi ni walimu wenye shahada tulioajiriwa Januari 2026 katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama. Tumekaa miezi minane tukisubiri malipo ya fedha za kujikimu na nauli, tukiamini kuwa hatimaye tutalipwa stahiki zetu.
Leo fedha zimefika, lakini tumelipwa TSh 250,000 pekee badala ya takribani TSh 950,000, pamoja na stahiki za nauli ambazo bado hatujalipwa.
Kwa kweli, hali hii imetuumiza sana. Tumekuwa tukivumilia kwa muda mrefu huku tukikabili gharama mbalimbali za maisha bila kupata fedha hizo. Tunajiuliza, fedha zilizotengwa kwa ajili ya stahiki zetu zimeishia wapi?
Tunaomba mamlaka husika, hususan Ofisi ya Rais–TAMISEMI na viongozi wa ngazi za juu, ichunguze suala hili na kutoa ufafanuzi wa kina kuhusu malipo hayo.
Hatupingi kulipwa; tunachodai ni stahiki zetu halali, zilipwe kwa uwazi na kwa mujibu wa taratibu za utumishi wa umma.
Hili si suala la fedha pekee, bali ni suala la haki, utu na kuthamini walimu wanaoitumikia nchi.