A
Anonymous
Guest
Habari gani wadau? Kama mnakumbuka, siku za nyuma kidogo kuna mdau alitoa dokezo kuhusu afisa elimu sekondari Kilwa kudhulumu sitahiki za walimu kama vile malipo ya likizo, malipo ya uhamisho na malipo ya UMISETA. Mdau alieleza hoja kadhaa kinagaubaga kuelezea uhalisia wa tuhuma zake kwa Afisa elimu huyo.
Ile mada ilivutia maana mimi mwenyewe ni mkazi wa Kilwa, hivyo nikataka kujua ukweli kuhusu tuhuma hizo.
Moja ya hoja katika tuhuma, ilikuwa kwamba kuna majina ya walimu ambao walikuwa katika mpango wa kulipwa nauli za likizo kama ilivyo utaratibu kwa watumishi wa umma wanakuwa na likizo moja ya kulipwa ndani ya miaka miwili yaliwekwa hadharani.
Kwa maelezo ya mdau yule ni kuwa walimu waliombwa taarifa zao kama vile account number na check number na waliziwasilisha. Lakini hadi mdau anaandika ile kero ni kuwa walimu walikuwa hawajalipwa.
Mimi niliwasiliana na baadhi ya walimu kiudadidisi sana ili kupata orodha ya majina ya walimu yaliyokuwa yametolewa kuwa watalipwa.
Sasa suala likawa ni kuthibitisha kama ni kweli bado hawajalipwa. Hivyo niliongea na walimu kadhaa waliokuwa kwenye ile orodha wakasema kuwa hawajalipwa na wanahisi kuwa pesa imeshapigwa.
Nikajisogeza kwa watumishi wa idara utumishi maana baadhi yao ni rafiki zangu pia. Nikaulizia kwa baadhi kuhusu yale malipo, Kwa maelezo yao ni kuwa kwa upande wao walikuwa wameshamaliza na kukabidhi kwa idara husika (hapa ni idara ya elimu sekondari). Nikagundua kuwa kumbe mdau aliyeandika ile kero hakuwa amekurupuka wala haukuwa uzushi.
Ukweli ni kwamba hadi leo tarehe 13/08/2024 walimu waliotakiwa kulipwa hawajalipwa. Na majina yalitolewa 28 Juni 2024. Na kwa Uthibitisho kutoka idara ya utumishi kilwa ni kuwa mkurugenzi alisaini mapema Julai.
Kwenye kufuatilia hili sakata nimegundua kuwa walimu wa sekondari Kilwa wanaomba likizo ya malipo halafu likizo nyingine ya kutakiwa kulipwa inawakuta bado hawajalipwa. Mfano kuna walimu waliomba likizo 2021 (ya malipo), halafu 2022 haohao walimu wakaomba isiyo ya malipo. Tena 2023 wakaomba ya malipo ilihali yale malipo ya likizo ya 2021 hawajalipwa. Pia kuna hawa walitakiwa kulipwa 2022 lakini tena wameomba likizo ya malipo 2024 wakiwa bado wanadai malipo ya 2022. Kwa ufupi uozo ni mwingi sana.
Tuhuma nyingine ilikuwa kuhusu malipo ya UMISETA. niliongea na baadhi ya walimu waliosimamia lile zoezi. Kwa maelezo yao ni kuwa waliwekwa kambini kilwa sekondari siku saba na wakapewa shilingi elfu hamsini (50,000) tena baada ya kudai sana. Halafu wakaenda Lindi Mjini wakawekwa kambini siku saba tena, wakalipwa shilingi laki moja (100,000).
Bahati mbaya sikubahatika kupata mawasiliano ya walimu wa wilaya nyingine za mkoa wa Lindi ili kulinganisha malipo. Lakini ukweli ni kama alivyoeleza Mdau yule kwenye andiko lake kuwa walimu walilipwa laki na nusu. Maana ikichukua jumla ya malipo wakiwa kilwa na malipo wakiwa lindi jumla ni hiyo 150k.
Kuhusu tuhuma za walimu wa kiume KIVINJE SEKONDARI kutembea na wanafunzi wao kama mdau alivyoeleza kwenye andiko lake, kuna ushahidi ninaukusanya. Ukikamilika nitakuja na uzi wake spesho siku za usoni na majina ya hao walimu na wanafunzi wanaotembea nao nitayabaisha yote.
Mwisho niombe vyombo husika vifanye uchunguzi wa kina kwa Afisa Elimu Sekondari Kilwa ili kama anaminya sitahiki za walimu achukuliwe hatua.