Tetesi: Walimu kupandishwa madaraja mwisho wa mwezi huu

Tetesi: Walimu kupandishwa madaraja mwisho wa mwezi huu

Acha kupinga,waraka ninao umesema walimu husika wapandishe,swala la kupanda madaraja liko kisheria halihusiani na bajeti,hujui kuwa mwezi wa tano watu walipanda madaraja,waweza niambia ni bajeti gani ilitumika kuwapandisha watu hao.

Hakika mama anaupiga mwingi,kura za watumishi wote hasa walimu lazima azibebe zote.jpm kabana sana watu,mama ni mwingi wa huruma,Mungu amjalie heri na baraka tele
Waraka au barua yenye maelekezo?
 

Attachments

  • maelekezo edited .jpg
    maelekezo edited .jpg
    114.7 KB · Views: 53
Mkuu Wewe sio mtumishi ,haya hayakuhusu,kukaa kimya nako ni busara,,swali gani hili
Ooh kumbe... Sasa si mngesema Uzi ni kwa ajili ya walimu pekee yao!

NB: Swali langu lililenga kujua kama hayo madaraja yana tija na kama hizo pesa hazitengenezi madai/madeni!

Nisamee digba sowey mtumishi
 
Kiambatisho kwenye barua yenye maelekezo
 

Attachments

  • kiambatisho kwenye maelekezo.png
    kiambatisho kwenye maelekezo.png
    179.9 KB · Views: 55
Tatizo sio umaskini na upuuzi wa walimu Bali ni dola iliamua KULINDA wanasiasa wanaovunja sheria na kukanyaga katiba !

Hivyo mwalimu hawezi tafuta Bunduki apambane na dola Ili kumpindua kiongozi anaesigina haki zao,Bali ni dola ndio inajukumu la kuchukua hatua pale haki za watu zinapovunjwa kwa kumtoa kiongozi madarakani kivyovyote vile!

Tuna dola inayochekelea WANASIASA wanaovunja sheria na haki za watu,hatujui ni kwanini labda kama Kuna maslahi wanapata toka kwa viongozi hao waovu!!!

Mwalimu asilaumiwe Kazi yake ni kutoa ujinga kwa vijana na anafanya vyema tangu uhuru!!
Umeongea vyema. Kuna nyakati ambazo watu hushuhudia uvunjifu wa sheria na hata katiba toka kwa viongozi na hakuna mtu wa kufanya kitu. Mfano kwa miaka kadhaa watumishi hawakuongezewa hata 100 ktk mishahara yao kinyume na sheria ya kazi iliyoweka increment kwenye mishahara, lakin hakuna mtu wa kupaza sauti kutetea wafanyakazi. Mfano tuliona watu wakipandishwa mishahara (madaraja Feb, 2016) lakini baadae wakapokwa pasipo hatia na wakaja kurejeshewa madaraja hayo Mwishoni mwa 2017 (wakiachwa nyuma na wenzao). Eti sababu iliyoelezwa ni uhakiki wa vyeti. Ila baada ya kuwapoka, hawakulipwa hata hizo arreas za kipindi walichosimamishiwa mishahara. Lakini hata Chama cha Walimu ambacho kinakata 2% ya Basic Salary ya Mwalimu @ mwezi wakikaa kimnya kabisa. Wao waliendelea tu kukata mshahara wa mwalimu ili wampe T-shirt siku ya mei mosi.

Kwa kweli kama Mama Samia ataamua kuwafuta Machozi hasa hawa walimu waliopunjwa madaraja na Wale waliowahi kunyang'anywa madaraja yao kwa kuwapa daraja angalau 1 juu, atakuwa amefanya jambo 1 kubwa sn kwao na atabarikiwa sn. Watumishi wamepitia kwenye dhuruma hapo katikati. Gharama za maisha zimepanda sana lakini kipato kimeganda kwa miaka.
 
Sasa mkuu au wewe ukisikia kupanda daraja unadhani nidaraja la kigamboni!? Hii mada haihusiani na walimu tu,mtumishi yeyote wa seikali akisikia kupanda daraja au cheo anajua maana yake,wewe sio mtumishi,kaa kwa kutulia
Ooh kumbe... Sasa si mngesema Uzi ni kwa ajili ya walimu pekee yao!

NB: Swali langu lililenga kujua kama hayo madaraja yana tija na kama hizo pesa hazitengenezi madai/madeni!

Nisamee digba sowey mtumishi
 
Kama ni haki yao na wanastahili wapandishwe tu, hii ni kisheria sema tu tunachukulia poa.
 
Wapewe tu hayo madaraja. Ni vile tu hamjui serikali inavyotamani kuboresha maslahi ya walimu tatizo wapo wengi.

Kada zipo nyingi sana zilizostopishwa kupanda madaraja lakini walimu hawanaga posho wala marupurupu zaidi ya mshahara, labda ndiyo maana serikali inawapa kipaumbele angalau wapunguze stress.

Unakuta dereva analipwa mshahara mdogo tu, lakini kwa mwezi anaingiza posho za safari zaidi ya mwalimu.

Pia tusisahau hawa walimu ndiyo wasimamizi wa uchaguzi.
 
Acha kupinga,waraka ninao umesema walimu husika wapandishe,swala la kupanda madaraja liko kisheria halihusiani na bajeti,hujui kuwa mwezi wa tano watu walipanda madaraja,waweza niambia ni bajeti gani ilitumika kuwapandisha watu hao.

Hakika mama anaupiga mwingi,kura za watumishi wote hasa walimu lazima azibebe zote.jpm kabana sana watu,mama ni mwingi wa huruma,Mungu amjalie heri na baraka tele
Una kichwa kigumu,hao waliopanda ni mwaka wa fedha ambao haujaisha.
 
Back
Top Bottom