Walimu kupiga watoto mpaka kuua! ipo siku atauliwa mtoto wa kiongozi ndipo tutaamka

Mtoa mada utasubiri sana, watoto wa wakubwa ni wakubwa pia, hawaogopi chochote.
Angalia yule aliyewatukana polisi mbele ya kamera na hakuna alichofanywa
 
Tatizo la wazazi mnaficha magonjwa ya watoto wenu,akiguswa na mwalimu kidogo inakuwa tiketi ya kifo na malalamiko kuanzia hapo,hakuna mwalimu wa kuchapa mtoto wa miaka 6 kwa jinsi hiyo inavyoelezwa never
Acha ujinga wewe mwalimu,madeni yanawafanya muwe na hasira sana
 
Jirani yangu mtoto wake wa form 4,ashapoteza jicho moja, baada ya mwalimu kumuadhibu na kipande cha fimbo kupiga jichoni, walimtekeleza mtoto KCMC huku mzazi akifichwa, amekuja kuambiwa na matron muda mrefu ushapita, wamekuja kusaidiwa na mkuu wa Wilaya baada ya mama wa mtoto kwenda kwake kuomba msaada, Shule wakalazimishwa kughalimia matibabu India, huko wakaambiwa mtoto amecheleweshwa sana, kuna uwezekano lisione tena.
 
Watoto wao wanasoma ulaya.

Hawa wetu wanaenda shule hawajala chochote tena upige fimbo tano, jua wewe umeshaua na utafungwa tu bure
 
Kwa bahati nzuri watoto wa sisi viongozi awasomi shule wanazo piga🤣🤣🤣

Mlipo ambiwa elimu GHARAMA mlibeza na mkachekelea elimu ya bure 🤣🤣🤣

Mtaisoma namba​
 
Uyo dogo alikua mgonjwa kabla ila tu hakuonyesha dalili za wazi, Huyu BTP mjinga alichokosea ni kumchapa mtoto mdogo kwa uchungu kama mwizi hii ilidhoofisha hali yake ya mwanzo sasa.
Me naweza sema Mzazi wa Mtoto na Mwalim wote wameshirikiana kuua. Issue ya mtu kuvunja damu we unampa panadol huoni ni Utaahira huo?

Angalizo, Oeni wanawake wenye akili na Walimu wawe na angalau dvn 1 ya 4m4.
 
Inaonekana mtoto alikuwa mgonjwa na alicheleweshwa kupata huduma sahihi za kiafya ila ndiyo hivyo tena jumba bovu limemwangukia teacher.
Huyo mwalimu hakwepi kosa lake.
Amehamsha magonjwa mengine.
Kwanza amekiuka kanuni ya adhabu ya viboko iliyowekwa na wizara husika.
Unapigaje mtoto kichwani?
Unapigaje mtoto wakati hujui historia yake ya afya?
Huyo kichaa akapigwe mjebele jela atatia akili.
 
Imeniuma sana. Sana yaani....

Lazima kesi za wanafunzi kudhuriwa na waalimu zitakua nyingi, ila zinafichwa.

Huyo mtoto hata kama alikuwa anaumwa, asingepigwa hivyo angekufa?

Mnaosema watoto wanakosa adabu, kuchelewa kuchukua namba ni kosa la kupigwa hivyo?

Hao waalimu ni wauwaji.

Post moterm inafanyika leo, lakini post moterm hazi-fojiki kweli? mimi siamini.

Kuna haja ya kudhibiti utoaji adhabu mashuleni.

Watoto hawadhuriwi kimwili tu, hata kiakili wanaweza kupata trauma.
 
Ushawahi kusikia mtoto amechapwa IST au Feza??
 
Hii inaskitisha sana,nikisoma habari za huyu mtoto na wengine kama yeye,waliokutwa na visa,hivi,machozi huwa yananitoka.Na pia ni muhimu,watu wanaopita karibu ya shule na wanaoishi jirani na shule,wakiona matukio kama haya,waende kuwatetea hawa watoto,mimi nikipita karibu ya shule,nikiona wanafunzi wanaadhibiwa na mwalimu au waalimu,lazima niingilie kati kuwatetea hawa wanafunzi.
Kwa nini kusianzishwe chama cha kuwatetea wanafunzi,na kiwe na matawi mpaka mashuleni na mpaka vyuoni?
 
Na hata kama hakudhurika sasa,huwenda atakapokuwa myu mzima,akapata madhara.Na nafikiri hii,ndio inapelekea mahospital kuwa na wagonjwa wengi,wamatatizo mbali mbali sugu,huwenda waliumizwa utotoni shule,kwa fimbo za kichwani,mgongoni,makalioni,mbavuni nk.
 
Actualy hakuna mtoto wa kingozi atauliwa, why hawasomi huko
 
Binafsi mimi siyo mwalimu , ila kuna namna waalimu wanachukuliwa poa. Hata hivo siungi mkono adhabu zilizo pitiliza.

Kwa miaka hivi karibuni wazazi kama wamekua wanawachagulia waalimu namna mtoto wake / wao aadhibiwe. Hii imepelekea walimu kutokua na time na shida zozote na wanafunzi . Saizi mwalimu anaangalia mambo yake tuu, mtoto aelewe ama asielewe , akosee ama asikosee hiyo haimuuhusu atajijua yeye na mzazi wake.
 
Shule wanazosoma watoto wa viongozi una uhakika kuna hao walimu?
 
Watoto sikuizi kama wazazi wao tuu wanajidai wanajua kila kitu .
 
wanawachagulia waalimu namna mtoto wake / wao aadhibiwe.
Ndio kuna namna mtoto anapaswa aadhibiwe.

Ukimpiga kama unampiga mwizi, ndo nini sasa?

Mwanao akipata changamoto za kiafya/akijeruhiwa kwa kupigwa shuleni utajisikiaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…