Walimu Mei mosi imekaribia, andaeni mabango ya maandamano ya Amani

Walimu Mei mosi imekaribia, andaeni mabango ya maandamano ya Amani

Mpwayungu Village

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2021
Posts
14,540
Reaction score
30,875
Time is too short, siku si nyingi sikukuu ya wafanyakazi inakuja. Je wewe kama mwalimu umejiandaaje? Umejiiandaa kuwa Chawa wa mama ili umsaidie ushindi 2025 kwenye box la kura au umejipanga kufanya harakati zenye Nia ya kumkomboa mwalimu kutoka kwenye ufukara wa kutia aibu.

Naomba tuende Sawa hapa : haki haiombwi, shairi la mwanalege kutoka Jamaica Peter toshi anasema watu wanataka kwenda mbinguni ila kufa hawataki. Sasa utaendaji mbinguni bila kufa. Ili haki ya mwalimu ipatikane lazima mrisk kazi zenu

Hiyo siku natamani muandamane barabarani mumwambie Samia kupanda madaraja ni kila baada miaka 3, muanze kupewa house allowance maana hamna hata nyumba za walimu, muanze kupewa teaching allowance ili kurahisisha shughuli za ufundishaji kama kudownload material mitandaoni na kununua teaching Aids

Sasa ipo hivi; kwenye haya maandamano wapo walimu watapoteza kazi, wapo watawashwa mbata na maaskari, wapo watakula kisago na wakuu wa shule maana huko mashuleni mkuu wa shule ni inversely proportion na walimu wenzake, mtatukanwa sana na watu wa CCM, cwt, TUCTA, tsc, mwijaku, Steve nyerere wote hao watakuwa upande wa mama maana asili ya wabongo bila kujipendekeza wanaona hawatoboi.

All in all move onnnnn, never quit please that day don't fall me down I beg you 🙏

No police force, no court, no government, no army, no anything will stop the will of the people. When Injustice becomes law resistance becomes duty (Thomas JF)
 
1/4 ya Wafanyakazi wa Serikali ni Walimu but Walimu hawawezi Ku influence chochote katika Serikali.Watu ambao wanaweza wakafanya maandamano na kusikizlizwa ni Madaktari na Manasi maana hao wasipofanya kazi watu watakufa
 
1/4 ya Wafanyakazi wa Serikali ni Walimu but Walimu hawawezi Ku influence chochote katika Serikali.Watu ambao wanaweza wakafanya maandamano na kusikizlizwa ni Madaktari na Manasi maana hao wasipofanya kazi watu watakufa
Mkuu walimu kwanza kitakachowasaidia ni wengi, maandamano ni watu hivyo watakapondamana nashauri pia wogome kuingia madarasani kufundisha
 
Kwanini uwe muoga kwenye kudai haki zako? Ivi unajua uoga unafedhehesha zaidi ya umasikini. Basi niwaambie tu mimi nitawadharau nasitawasalimia mpaka mtakapoandamana kudai haki zenu

Walimu wengi wana miaka zaidi ya kumi kazini ila wakiomba uhamisho hawapewi na vigezo wanavyo, uhamisho wa kubadilisha pia ni mbinde majina yanatoka ila vibali havitoki, una Miaka kumi na mbili ila umepanda daraja Mara moja tu, pesa yako ya kujikimu mpaka Leo hujamaliziwa unapewa nusu nusu, mshahara wako wa kwanza mpaka Leo hujalipwa unadai malimbikizo hata mfuko wa shangazi kaja unajaa, mnakaa kwenye magofu, Mnaishi Kwa kutukanwa, mnapigwa biti na mkuu wa shule mnapwaya, Mnaishi Kwa huzuni kama yatima, mna madeni yasiyoisha, mishahara yenu niyamiaka kumi nyuma Dunia ya sasa kupewa laki tano ni matusi, hamna posho yoyote, hata kununua pikipiki tu mpaka ukope maana kusave million Tatu na Familia uliyonayo haiwezekani.

Walimu walimu please Mei mosi nataka muandamane, nataka walimu mdai haki zenu. Vinginevyo nitawadharau mpaka kufa mmekuwa waoga kama ngiri jamani.

Halafu pendaneni muwe kitu kimoja hakuna mapinduzi bila umoja. Mkuu wa shule akileta ukuda mpigeni spana za kutosha kwenye vikao vyenu mpaka ajihisi kajinyea

Acheni woga hakuna wakuwakomboa zaidi ya kujikomboa nyinyi wenyewe, lazima ifike wakati mseme enough is enough
 
Back
Top Bottom