Walimu Mei mosi imekaribia, andaeni mabango ya maandamano ya Amani

Walimu Mei mosi imekaribia, andaeni mabango ya maandamano ya Amani

Kwanini uwe muoga kwenye kudai haki zako? Ivi unajua uoga unafedhehesha zaidi ya umasikini. Basi niwaambie tu mimi nitawadharau nasitawasalimia mpaka mtakapoandamana kudai haki zenu

Walimu wengi wana miaka zaidi ya kumi kazini ila wakiomba uhamisho hawapewi na vigezo wanavyo, uhamisho wa kubadilisha pia ni mbinde majina yanatoka ila vibali havitoki, una Miaka kumi na mbili ila umepanda daraja Mara moja tu, pesa yako ya kujikimu mpaka Leo hujamaliziwa unapewa nusu nusu, mshahara wako wa kwanza mpaka Leo hujalipwa unadai malimbikizo hata mfuko wa shangazi kaja unajaa, mnakaa kwenye magofu, Mnaishi Kwa kutukanwa, mnapigwa biti na mkuu wa shule mnapwaya, Mnaishi Kwa huzuni kama yatima, mna madeni yasiyoisha, mishahara yenu niyamiaka kumi nyuma Dunia ya sasa kupewa laki tano ni matusi, hamna posho yoyote, hata kununua pikipiki tu mpaka ukope maana kusave million Tatu na Familia uliyonayo haiwezekani.

Walimu walimu please Mei mosi nataka muandamane, nataka walimu mdai haki zenu. Vinginevyo nitawadharau mpaka kufa mmekuwa waoga kama ngiri jamani.
Halafu pendaneni muwe kitu kimoja hakuna mapinduzi bila umoja. Mkuu wa shule akileta ukuda mpigeni spana za kutosha kwenye vikao vyenu mpaka ajihisi kajinyea

Acheni woga hakuna wakuwakomboa zaidi ya kujikomboa nyinyi wenyewe, lazima ifike wakati mseme enough is enough
Umeshapata Basha kwenye Ile thread sasa umekuja kwa Kasi ya mwanga kuwasiginia kunguni walimu
 
Kama hiyo 500k ni nyingi, mbona mnamaisha magumu sana...
Mikopo, bond, kuombaomba mnaongoza nyie walimu..
Halafu kazi gani hyo kila siku matukio ya kutatanisha yanafanywa na walimu?..

Mnapoambiwa ukweli msikasirike na mkumbuke haya tunayoandika mama Samia anasoma, sisi tunawasaidia nyie mfikiliwe halafu wewe unapotosha wenzio.
 
Back
Top Bottom