Walimu mnaweza kujiajiri

MAHANJU

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2014
Posts
5,252
Reaction score
8,003
Habarini walimu wenzangu!

Mimi kama mwalimu mwezenu nataka niwashauri kitu kimoja; Naombeni niwaambie kua msiwe na akili tegemezi kiasi hichi kwenye ajira toka serikalini.

Nimemaliza shahada ya ualimu wa masomo ya sanaa miaka 5 iliyopita, Lakini baada ya kumaliza masomo tu tuliungana vijana 6 tuliomaliza vyuo vya walimu toka maeneo mbalimbali wakati huo, wawili kati yetu walikua wahitimu wa diploma, Hatukua na zana yeyote mikononi!

Bila kujali baada ya muda mfupi kutakua na ajira toka serikalini Tulianzisha vituo vya kufundisha tuition, tukaweka malengo, Hakika tulifanikiwa sana kukusanya pesa nyingi sana japo kulikua na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na wawili kati yetu kuamua kwenda serikalini, moja kwenye siasa na kubakia watatu tu kuendelea na mbio za malengo yetu, baadaye tuliamua kusimamisha majengo yetu wenyewe ya tuition I kwa pesa tulizokua tunakusanya.

Tulizidi kujipanga vizuri na hatimaye kuongeza majengo, tukabadili mawazo ya tuition tuanzishe shule au chuo tutafute usajili tusonge mbele! Tuliendelea kuongeza idadi ya majengo kwa tulichokua tukikipata na tulipopelewa pesa tulienda bank kukopa na tukawa tunapeleka narejesho kila mwezi.

Sio siri tulifanikiwa kufungua chuo cha ualimu kwa ngazi ya cheti na stashahada na tukapata usajili serikalini, ninavyoongea hivi sasa Leo chuo chetu kinapaa hapa mkoani Arusha,Tumetoa ajira kwa wafanya kazi 17, na kati yetu kwa wale waliokua na degree kila moja ana masters nikiwemo Mimi Nina masters ya biashara na nataka kufanya PHD mwaka huu, wale waliokua na diploma leo ni degree holders.

Vijana msilale kusubiri ajira serikalini! Tumieni fursa zipo nyingi.
 
arusha chuo gani unamiliki mkuu naomba jina la chuo tusije tukawa tunapigana kamba hapa
 
kweli unachokisema lkn changamoto hapa ni kujaribu,,watu wanaogopa kuharibu wakati kujiajiri ndiyo mpango mzma,hizi ajira za serikali zinasumbua sana tutakalia kunyosheana vidole badala ya kufanya kazi
 
Huu ndio ujinga tunaoukalia watanzania, Ufinyu wa kufiri ndio unawafanya muendelee kuwaza serikali uwaletee ajira,Yaani mimi nakuelekeza njia za kutoka unaleta upumbavu wako hapa! Huna haja ya kusaidiwa kalia upuuzi wako huo wa kuchangia sabuni ya kuogea na wadogo zako huku ukisubiria ajira serikalini. Ndio maana walimu tunadharauliwa kila siku.
 
Mawazo kuntu kwa watu butu. Ndiyo maana unaona komenti 2 za mwanzo ni za matusi. Watz hawataki kusikia au kuambiwa juu ya kujiajiri. Wataka kuajiriwa.

Hongera sana mtoa mada lkn nakupa pole maana utapokea mitusi mingi humu. Siyo kwasabb ulichoongea hakina maana, la! Kina maana sana kakini walaji ndiyo tatizo.
 
Mkuu hapa sio facebook.
Hapa ni JF where we dare to talk openly.
Leta ushahidi tuamini habari yako.
 
kweli unachokisema lkn changamoto hapa ni kujaribu,,watu wanaogopa kuharibu wakati kujiajiri ndiyo mpango mzma,hizi ajira za serikali zinasumbua sana tutakalia kunyosheana vidole badala ya kufanya kazi

Mkuu ni kujaribu kidogo kidogo, Sisi sote tuliajiriwa lakini walioenda serikalini ni watatu kati ya 6 tulioanzisha program na tofauti yetu ya kimaisha kwa sasa ni kubwa.
 
Mkuu hapa sio facebook.
Hapa ni JF where we dare to talk openly.
Leta ushahidi tuamini habari yako.

anashindwa kututajia jina la chuo chake ndio uamini huyu ni mwongo wa waongo. kitu kutaja tu jina anapata kigugumizi.
 
ni mwongo na kama sio mwongo basi ataje jina la hicho chuo chake tuamini kwa hayo aliyoyaandika maana kuna watu wanajua sana kutunga stori

anaweza kuwa muongo kweli aisee!!!

maana hakuna uwekezaji lahis hivyo hata kama ni wakala wa freemanson hayo mafanikio kwa 5 years napata mashaka.

basi tunamuomba ataje chuo mbona hakitaji hata magaid wanataja jina la vikundi vyao whay not yeye anaogopa
 
Chuo gani hicho mlichoanzisha mbona hujaweka ata jina tujue km usemayo yana ukweli ndani yake au ni story za abunuasi tu
 
MAHANJU , ni ushauri mzuri sana lakini umeutoa katika muda na mazingira yasiyo sahihi.
 
Last edited by a moderator:
MAHANJU , ni ushauri mzuri sana lakini umeutoa katika muda na mazingira yasiyo sahihi.

Mkuu naelewa sana kua kuna watu ni very stressed na kusubiri ajira za gvt, Mimi nimekaa Kenya miaka mitatu, nimejifunza jinsi wenzetu wana ticha katika, Nilisema nikimaliza masomo tu sitasubiri ajira lazima nikachakarike na leo hii nimeshakomaa sana kimawazo kulinganisha na umri wangu.Watanisamehe sana wanaonitukana humu kwa sababu tu nimeweka kastory cha safari ya maisha yangu.
 
Last edited by a moderator:
Acha kuwashauri wenzio ujinga . kwa Nchi hii kitu kama hicho hakiwezekani wew.
 
hahahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!! Ila siku ya leo nlichokiona humu ni unforgetable. Mbavu zangu jaman mweeeeeeeeeee mnaniuaaaaaaaaa! Ila kuhusu ajira nna hakika mei mosi nimehakikishiwa na mtumishi mmoja wa tamisemi dom bado wanapanga majina believe me.
 
Mtoa maada wewe ni sawa na mtu kaenda mcbani then ndo unahutubia wafiwa kuwa marehem alikufa kizembe hapo c dhan kama utapata positive reaction
 
CHUO KINAITWAJE MKUU, DOGO ANATAKA KUJA KUSOMA...TUTAJIE BASI hatutaki ahad kama SirGin sisi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…