MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,252
- 8,003
Habarini walimu wenzangu!
Mimi kama mwalimu mwezenu nataka niwashauri kitu kimoja; Naombeni niwaambie kua msiwe na akili tegemezi kiasi hichi kwenye ajira toka serikalini.
Nimemaliza shahada ya ualimu wa masomo ya sanaa miaka 5 iliyopita, Lakini baada ya kumaliza masomo tu tuliungana vijana 6 tuliomaliza vyuo vya walimu toka maeneo mbalimbali wakati huo, wawili kati yetu walikua wahitimu wa diploma, Hatukua na zana yeyote mikononi!
Bila kujali baada ya muda mfupi kutakua na ajira toka serikalini Tulianzisha vituo vya kufundisha tuition, tukaweka malengo, Hakika tulifanikiwa sana kukusanya pesa nyingi sana japo kulikua na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na wawili kati yetu kuamua kwenda serikalini, moja kwenye siasa na kubakia watatu tu kuendelea na mbio za malengo yetu, baadaye tuliamua kusimamisha majengo yetu wenyewe ya tuition I kwa pesa tulizokua tunakusanya.
Tulizidi kujipanga vizuri na hatimaye kuongeza majengo, tukabadili mawazo ya tuition tuanzishe shule au chuo tutafute usajili tusonge mbele! Tuliendelea kuongeza idadi ya majengo kwa tulichokua tukikipata na tulipopelewa pesa tulienda bank kukopa na tukawa tunapeleka narejesho kila mwezi.
Sio siri tulifanikiwa kufungua chuo cha ualimu kwa ngazi ya cheti na stashahada na tukapata usajili serikalini, ninavyoongea hivi sasa Leo chuo chetu kinapaa hapa mkoani Arusha,Tumetoa ajira kwa wafanya kazi 17, na kati yetu kwa wale waliokua na degree kila moja ana masters nikiwemo Mimi Nina masters ya biashara na nataka kufanya PHD mwaka huu, wale waliokua na diploma leo ni degree holders.
Vijana msilale kusubiri ajira serikalini! Tumieni fursa zipo nyingi.