Asango
JF-Expert Member
- Mar 24, 2011
- 234
- 25
Wakati wanalalamika makato ni makubwa sana,Serikali kwa ushirikiano na Cwt wameamua kuanzisha Bodi ya kitaalam ya Waalimu na ni ya Kisheria.Inaitwa Tanzania Teachers Professional Board Act 2013.
Bodi hii itasimamia utaalam wa walimu ni nidhamu kwa ujumla.Malengo ni haya yafuatayo
1.kuhakikisha usimamizi wa Elimu unaongozwa na utaalamu.
2.kuweka viwango sawia vya kitaalamu vinavyosimamiwa na chombo kimoja kitakachotambulika kitaifa na kimataifa.
3.kuinua hadhi ya waalimu pamoja na kuboresha viwango vya kufundisha na kujifunza.
Bodi hii itaendeshwa kwa michango ya wanachama na wahisani mbalimbali.
Kutakuwa na Registration fee na Annual fee kwa wanachama ambao ni walimu wa shule za umma na binafsi.
Swali langu
Je, uanzishwaji wa Bodi hii unaimanisha kwmb TSD na CWT zitaondolewa?
Na kama cwt ndo waliomba kuanzishwa kwa bodi hii kwa nini Wasiendeshe bodi hii kwa kutumia zile 2% na vitega uchumi kuliko kuendelea kuwakata waalimu na hali yao duni?
Mdau wa Elimu nchini mnamaoni gani kuhusu jambo hili?
Mpango wa uanzishwaji wa Bodi hii umeigwa kutoka ktk nchi ya Nigeria.