Walimu ni wasumbufu sana

Walimu ni wasumbufu sana

incredible terminator

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2016
Posts
2,498
Reaction score
4,162
Jaman kusema kweli ni wazi kuwa asilimia 99% ya wana JF tumepitia maisha ya shule sipendi kutetea kuwa hamna wanafunzi wakorofi ila pia kuna mazingira mengne ya migomo ambayo huchangiwa na walimu pia kutokana na na kauli zao kwa wanafunzi natoa mfano huu wa kweli nikiwa na iman na kauli yangu na nikiamini uwepo wa mungu kuwa sidanganyi[emoji16]

Juzi nilienda shule fulani (mkihitaji nitaitaja kwa jina) mkoa wa Mbeya nikawa na shida ya kumwona mwalimu fulan kiofsi hali ambayo ilinifanya nimfuate ofisini....

Binafsi mwalimu yule hanijui na hakuwahi kujua kama awali niliwahi kusoma shule hiyo nilivyoingia niliulizia jina husika kwa mwalimu mwenzake na aliponionesha nikaamua kumfuata mezani pake ila cha ajabu muda wote huo mwalimu huyo alikuwa yupo bize na laptop yake hata hakuweza kuinua macho na kuniangalia usoni kuwa anaemwongelesha ni nani maongezi yetu yalikuwa hivi kwa mda wote huo mwalimu akiwa haniangalii usoni,,,,,

MIMI: Mwalimu shkamoo

MWL: Kimya.......(bize na lapt0p)

MIMI: Mwalimu pole na majukum nilikuwa na shida naww ila samahan kwa usumbufu......[emoji24] [emoji24] [emoji24]

MWALIMU: (bila ya kuniangalia uson) Una shida gani na hayo majukumu unayonipa pole umeyaona wap?

MIMI: Mwl samahan kama nimekuudhi basi ila nina haki ya kusikilizwa nami pia[emoji24] [emoji24]

MWALIMU: (Kwa hasira kali bila kuniangalia) unasemaje mpumbav mkubwa ww kamjibu hivyo mama yako....(mara anageuka anakuta siyo sura ya mwanafunzi kama alivyodhania)[emoji15] [emoji15] [emoji15]

MWALIMU:[emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] (kwa mshangao huku walimu wenzake wametugeukia wote baada ya kusikia lugha ile ya jazba!!!

MWALIM: OOOh Mr samahani nikajua ni haya majinga yanayotusumbua karibu [emoji23] [emoji23] [emoji23]

MIMI: Nikamwelezea shida yangu alivyonisikiliza nikaamua kuondoka"

Sasa fikilia angekuwa mwanafunzi pale na anashida ya kuonana na Mwl wa zamu ili asaidiwe unadhanu kipi kingefuatia pale kama siyo mvua ya viboko kwake maskini mwanafunzi bila hata kosa???

Walimu badilikeni mnaishi na watoto wa wazazi wenzenu!
 
WALIMU wakiomba teaching allowance Vigogo wa wizara wanajifanya hawasikii, wakitoa kichapo wanatafutwa!!!
 
Inahusiana na nini na post yangu hapo??? Au ww ni moja ya wanaotetea ujambaz mwanafunzi ana be treated kama mnyama huku unajikuta umesomea psychology ya watoto huo ni upuuzi mtupu
Kwa hiyo unatakaje, alikuwa busy anaandaa kipindi, wewe vipi bhana!!
 
1475879298863.jpg
Acheni unafiki wote wenye mihemko ya kutetea hawa boko haram imagine huyu ni mwanao ww ungejiskiaje
 
WALIMU wakiomba teaching allowance Vigogo wa wizara wanajifanya hawasikii, wakitoa kichapo wanatafutwa!!!


Wananyimwa teaching allowance huku wengine wanapewa sitting allowance
 
HUU MWEZI NAONA UNALALA NA WALIMU TU................ HADI MWEZI UISHE AU LITOKEE LINGINE LA KUZIBA LA MBEYA, WALIMU WATAKUWA WAMEPUNGUA SANA KILO.
Hii ndo Tz yetu inaendeshwa na matukio
 
tusha jua mnampango wa kuto wapandisha walimu madaraja na posho
 
Inahusiana na nini na post yangu hapo??? Au ww ni moja ya wanaotetea ujambaz mwanafunzi ana be treated kama mnyama huku unajikuta umesomea psychology ya watoto huo ni upuuzi mtupu
"Ana be treated" ndio kitu gani!?
 
Kwa walimu wote tz, mungu awaongezee moyo wa uvumilivu, na ustahimilivu
 
Back
Top Bottom