GE2025 Walimu Rukwa wahimizwa kujitokeza kupiga kura oktoba 29

GE2025 Walimu Rukwa wahimizwa kujitokeza kupiga kura oktoba 29

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Chama cha Walimu Mkoa wa Rukwa (CWT) kimewahimiza walimu wote kushiriki kikamilifu katika zoezi la upigaji kura linalotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa CWT Mkoa wa Rukwa, Mwalimu Doseph Ndalama, amesema chama hicho kinaendelea kushirikiana kwa karibu na serikali katika masuala mbalimbali ya maendeleo ya elimu, hivyo amewataka walimu kupuuza taarifa potofu zinazoenezwa kuhusu uchaguzi huo.

Mwalimu Ndalama amesema ni haki ya kikatiba kwa kila raia kushiriki katika uchaguzi, kwani ni njia muhimu ya kuchagua viongozi wanaowaletea maendeleo.

Ameongeza kuwa, wananchi wa Mkoa wa Rukwa na Watanzania kwa ujumla wanapaswa kutumia fursa ya uchaguzi kwa amani na utulivu, badala ya kususia au kujiingiza katika vitendo vya vurugu wakati wa mchakato huo.
 
Back
Top Bottom