Walimu Sekondari ya Aga Khan wagoma kisa Ubaguzi wa Rangi

Muhimbili ipo kwanini unganganie Agakhan?
 
Mbona kwenye habari wanasema ni wageni...Hivi CWT wana msaada kweli?
 
Ukishakaa na Rostam Aziz akasema sio Mtz?
Tatizo mnapenda bagua ndo maana mnabaguliwa

Ni kinyune chake, Watanzania wanabaguliwa kwenye nchi yao kwa sababu siyo wabaguzi au Watanzania ni dhaifu na wanashindwa kujiweka kwanza kama tungejipendelea sisi tusingebaguliwa.

Kwa hiyo unaamini kabisa Rostamu anajiona Mwafrika na anakuthamini? Unajua kwa nini Kampuni yake kaiita Caspian? Watu kama wewe ndio sababu ya Watanzania kubaguliwa na kulia lia kubaguliwa kila siku na kila mahali kwenye Nchi yao wenyewe, mlipigania Manji hivyo hivyo leo hii Manji yuko wapi kama alikuwa ni Mtanzania na aliwathamini?
 
Wewe umeenda mara nyingi kufanya nini au una tatizo na kiafya?
 
Hakuna atakayewasikia, na wala hakuna anayejali.

Poleni
 
Daah, nimesoma hapo 2003 - 2006. Ila Sikuwahi kukutana na ubaguzi wa rangi kiukweli, labda kama ndio wameanza sasa.

Ila nilichogundua kwa wanafunzi wa kihindi ni wivu kwa wenzao waKiafrika pale wanapofanya vizuri zaidi yao kwenye mitihani. Yaani ukishika namba moja darasani basi utaona wanavyokuangalia kwa jicho la husda, yaani ni kama hawategemei Muafrika awe bright kuliko wao
 
Huu unaguzi wa ndani ya nchi utaisha pale Watanzania tutakapo wacha kulalamika na tuchukue hatua
Una akili sana kongole. Shida ipo hapo sisi niwatu wakubofya kibodi tu na kulalamika mitandaoni but ukija mitaani sisi ndowakwanza kuwashobokea hususani dada zetu hawa yani wanawashobokea sana wahindi
 
Hapo hutasikia mwanaharakati yeyote akipaza sauti kukumea haya maonevu coz hawana maslahi na hao waalimu hii ndio Tanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…